KLABU ya Manchester United imepiga hatua katika kutafuta suluhisho la safe yake ya ulinzi baada ya kukubali kutoa Pauni Milioni 24 kumnunua beki wa kati wa Atletico Madrid, Miranda.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 29 alicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa timu yake ikifungwa dakika za nyongeza na Real mjini Lisbon Jumamosi.
Miranda alikuwa nguzo muhimu katika safe ya ulinzi ya timu ya kocha Diego Simeone iliyotwaa ubingwa wa Hispania, La Liga na sasa yuko njiani kuhamia kikosi cha Louis van Gaal Uwanja wa Old Trafford, baada ya kupewa ofa ya Mkataba wa miaka minne.
Kisiki: Mbrazil huyo alikuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Diego Simeone kilichotwaa taji la La Liga
WASIFU WA MIRANDA
UMRI: Miaka 29
UREFU: Futi 6 na inci 1
NAFASI: Beki wa kati
KLABU: Atletico Madrid
MECHI ALIZOCHEZA MSIMU ULIOPITA: 45
MECHI ALIZOICHEZEA BRAZIL: 7
Ajabu sana kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari hajamchukua beki huyo katika kikosi chake cha Kombe la Dunia licha ya Miranda kuonyesha kiwango kizuri siku za karibuni.
Gazeti la Hispania, AS limesema kwamba beki huyo alikuwa Jijini Manchester kutafuta shule katika kuelekea kukamilisha mango wake huo wa kuhamia klabu hiyo.
Van Gaal amesema ana tatizo la safu ya ulinzi katika timu hiyo hususan, baada ya kuondoka kwa Rio Ferdinand na Nemanja Vidic.
Na Miranda, licha ya umri wake mkubwa anabaki kuwa chaguo salama baada ya kazi nzuri aliyoifanya tangu ametua Vicente Calderon miaka mitatu iliyopita.
0 comments:
Post a Comment