Na Renatus Mahima, Mbeya
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameahidi neema kwa wakazi wa jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwa kuukarabati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa ili utumike kwa mechi za kiamataifa za mashindano.
Mara tu baada ya mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwenye uwanja huo jijini hapa, aliahidi neema kwa wakazi wa jiji la Mbeya kwamba atazungumza na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ili uwanja huo utumike kwa mashindano ya kimataifa ya soka.
Malinzi, aliyeingia madarakani Oktoba 28 mwaka jana akichukua mikoba ya mtangulizi wake katika shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini, Leodegar Tenga, alisema atahakikisha Taifa Stars inacheza katika maeneo mengi zaidi nchini ukiwamo mkoa wa Mbeya.
"Lengo langu ni kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanaishuhudia timu ya taifa ikicheza katika maeneo ya kwao. Tuko katika mkakati kabambe wa kuhakikisha viwanja vingi nchini vinakarabatiwa na kukidhi vigezo vya kimataifa. Nitazungumza na FIFA ili waje kuukagua Uwanja wa Sokoine utumike kwa mechi za kimataifa za mashindano," alisema Malinzi.
"Tayari wataalam wa FIFA wako nchini kwa ajili ya kuweka nyasi bandia kwenye viwanja mbalimbali nchini. Nitazungumza nao ili uwanja huu pia upate fursa hiyo," aliongeza Malinzi.
Suleiman Haroub, katibu mkuu wa Chama cha Soka mkoani Mbeya (MREFA) aliiambia BIN ZUBEIRY mjini hapa jana kuwa wamekubaliana na TFF kuufanyia marekebisho Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ili ukidhi vigezo vya kimataifa.
"TFF wameahidi kutusaidia, ni habari njema kwa wakazi wa Mbeya, tunaanza kwa kufanya ukarabati mkubwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, baadaye tutaboresha maeneo mengine," alisema Haroub.
Juzi alfajiri mtaalamu wa nyasi bandia kutoka (FIFA), Ian McClemen aliwasili nchini kwa ziara ya siku tatu na mara tu baada ya kutua jijini Dar es Salaam, alikwenda mjini Bukoba, Kagera kukagua Uwanja wa Kaitaba na jana alikwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Kwa mujibu wa Boniface Wambura, ofisa habari na mawasiliano wa TFF, viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa 'Goal Projects'. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liteue mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameahidi neema kwa wakazi wa jiji la Mbeya na vitongoji vyake kwa kuukarabati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa ili utumike kwa mechi za kiamataifa za mashindano.
Mara tu baada ya mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwenye uwanja huo jijini hapa, aliahidi neema kwa wakazi wa jiji la Mbeya kwamba atazungumza na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ili uwanja huo utumike kwa mashindano ya kimataifa ya soka.
Malinzi akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Mbeya juzi |
"Lengo langu ni kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanaishuhudia timu ya taifa ikicheza katika maeneo ya kwao. Tuko katika mkakati kabambe wa kuhakikisha viwanja vingi nchini vinakarabatiwa na kukidhi vigezo vya kimataifa. Nitazungumza na FIFA ili waje kuukagua Uwanja wa Sokoine utumike kwa mechi za kimataifa za mashindano," alisema Malinzi.
"Tayari wataalam wa FIFA wako nchini kwa ajili ya kuweka nyasi bandia kwenye viwanja mbalimbali nchini. Nitazungumza nao ili uwanja huu pia upate fursa hiyo," aliongeza Malinzi.
Suleiman Haroub, katibu mkuu wa Chama cha Soka mkoani Mbeya (MREFA) aliiambia BIN ZUBEIRY mjini hapa jana kuwa wamekubaliana na TFF kuufanyia marekebisho Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine ili ukidhi vigezo vya kimataifa.
"TFF wameahidi kutusaidia, ni habari njema kwa wakazi wa Mbeya, tunaanza kwa kufanya ukarabati mkubwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, baadaye tutaboresha maeneo mengine," alisema Haroub.
Juzi alfajiri mtaalamu wa nyasi bandia kutoka (FIFA), Ian McClemen aliwasili nchini kwa ziara ya siku tatu na mara tu baada ya kutua jijini Dar es Salaam, alikwenda mjini Bukoba, Kagera kukagua Uwanja wa Kaitaba na jana alikwenda jijini Mwanza kukagua Uwanja wa Nyamagana.
Kwa mujibu wa Boniface Wambura, ofisa habari na mawasiliano wa TFF, viwanja hivyo vinawekwa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa 'Goal Projects'. Baada ya ukaguzi huo, McClemen atatuma ripoti yake FIFA ili shirikisho hilo liteue mkandarasi wa kufanya kazi hiyo.
Kwa Tanzania viwanja vilivyowekwa nyasi bandia hadi sasa kupitia Goal Project ni Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.
0 comments:
Post a Comment