TIMU ya Taifa ya Malawi (Flames) imewasili jijini Mbeya tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Mei 4 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Flames ikiwa na msafara wa watu 31 imewasili jana (Mei 1 mwaka huu) saa 1 jioni kwa njia ya barabara, na imefikia hoteli ya Manyanya. Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo jijini Mbeya tangu Aprili 27 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo.
Kiingilio katika mechi hiyo kitakuwa sh. 5,000 wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.
Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.

0 comments:
Post a Comment