// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MABAO SABA YATINGA NYAVUNI UFUNGUZI MICHUANO MIPYA CECAFA, MBEYA CITY YAANZA KAZI LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MABAO SABA YATINGA NYAVUNI UFUNGUZI MICHUANO MIPYA CECAFA, MBEYA CITY YAANZA KAZI LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, May 24, 2014

    MABAO SABA YATINGA NYAVUNI UFUNGUZI MICHUANO MIPYA CECAFA, MBEYA CITY YAANZA KAZI LEO

    Na Rodgers Mulindwa, KHARTOUM
    MABAO saba yametinga nyavuni katika mechi za ufunguzi za michuano ya mipya ya klabu ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) iitwayo Nile Basin jana nchini Sudan.
    Victoria University ya Uganda imeilaza 1-0 Malakia ya Sudan Kusini, wenyehi Al-Merreikh wameichapa 3-0 Polisi ya Zanzibar na wenyeji wengine, Al-Shandi wameilaza 2-1 Dkhill ya Djibouti.
    Mbeya City wanaanza kazi leo Sudan

    Wawakilishi wa Tanzania Bara, Mbeya watacheza mechi yao ya kwanza leo na Academie Tchite ya Burundi Saab 11:30 jioni kabla ya AFC Leopards ya Kenya kumenyana na Enticelles ya Rwanda Saa 2:00 usiku katika mchezo wa Kundi B.
    Michuano hiyo inashirikisha mabingwa wa Kombe la FA na washindi wa pili wa Ligi Kuu wa nchi wanachama wa CECAFA. Mbeya City imechukua nafasi ya Azam FC, washindi wa pili wa Ligi Kuu msimu uliopita, ambao wamejitoa.
    Simba SC ambao wangechukua nafasi ya Azam, wakati taarifa inakuja ya kufanyika kwa mara ya kwanza michuano hiyo, walikuwa wamekwishavunja kambi na wachezaji wao wote walikuwa wameruhusiwa likizo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MABAO SABA YATINGA NYAVUNI UFUNGUZI MICHUANO MIPYA CECAFA, MBEYA CITY YAANZA KAZI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top