MSHAMBULIAJI Rickie Lambert amewasili Liverpool kufanyiwa vipimo vya afya kuelekea kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 4 kutua Merseyside.
Mpachika mabao huyo Southampton, ambaye hakutumika jana England ikiichapa 3-0 Peru katika mchezo wa kirafiki, alitemwa na Wekundu hao akiwa na umri wa miaka 15.
Sasa Lambert anakwenda kuungana na kikosi cha Brendan Rodgers, iwapo atakamilisha vipimo bila tatizo.
Yuko njiani: Rickie Lambert (kushoto, pembeni ya Adam Lallana, ametua Liverpool kufanyiwa vipimo vya afya
Dau la uhamisho la Pauni Milioni 4 litaongezeka kulingana na idadi ya mechi atakazokuwa anacheza.
Lambert, ambaye alianzia soka yake katika akademi ya Liverpool, atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo katika dirisha hili linalotarajiwa kuwa la kishindo.
Anaweza kufuatiwa na wachezaji wenzake aliokuwa nao Southampton, katokana na Liverpool kuwa katika mango wa kuwasajili Adam Lallana mwenye thamani ya Pauni Milioni 25 na Dejan Lovren ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.
0 comments:
Post a Comment