// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KIZA KINENE CHATOWEKA UCHAGUZI MKUU SIMBA, SASA NURU YAANGAZIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KIZA KINENE CHATOWEKA UCHAGUZI MKUU SIMBA, SASA NURU YAANGAZIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, May 05, 2014

    KIZA KINENE CHATOWEKA UCHAGUZI MKUU SIMBA, SASA NURU YAANGAZIA

    Na Salma Juma, Dar es Salaam 
    UCHAGUZI mkuu wa klabu ya Simba sasa umeanza kunukia baada ya Katiba ya timu hiyo kukamilika huku Kamati ya uchaguzi ikitarajiwa kukutana kesho kwa ajili ya kujadili tarehe rasmi ya kuanza mchakato wa uchaguzi huo.
    Kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Damas Ndumbalo inatarajia kukutana kesho, kujadili mchakato mzima wa uchaguzi wa klabu hiyo ambao awali ulipangwa kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
    Katiba ya Simba ambayo imefanyiwa marekebisho tayari imekabidhiwa jana kwa uongozi wa klabu hiyo kutoka kwa Serikali baada ya kupitiwa kifungu kwa kifungu na kuridhika nayo.

    Awali katiba hiyo ilionekana kuwa na mapungufu na kulazimisha kuipitia upya ili kuondoa mapungufu hayo, huku Mkurugenzi wa Michezo Leornad Thadeo akionekana kufanya kazi nzuri baada ya Simba kuirejesha Ijumaa ya wiki iliyopita.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema kuwa tayari wamekabidhiwa Katiba ambapo kesho watakutana na kamati ya Uchaguzi kupanga mchakato mzima wa uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo.
    Kamwaga amesema, baada ya kamati kukutana leo, taratibu nzima za mchakato huo, zitawekwa wazi kesho, na kuwapa fursa wagombea kuanza mchakato huo.
    Alisema kuwa katiba yao imepitisha kuwepo kwa Kamati ya Maadili na Rufaa ambazo Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage atazitangaza wiki ijayo huku pia katiba ikipendekeza kuwepo kwa mgombea mmoja mwanamke wa kuchaguliwa.
    Kamwaga alisema, vipengele vyote vimepita katika katiba yao, isipokuwa cha ibara ya 26(4) kuhusu sifa za mgombea.
    “Katiba ya sasa ni lazima katika wagombea watano wa kamati ya utendaji nafasi moja awepo mwanamke, hivyo basi nawaomba wanawake mwenye sifa wajitokeze kwa wingi kuwania uongozi ndani ya Simba, na pia wanaweza hata wakawa watatu, lakini nafasi moja ni lazima,”alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KIZA KINENE CHATOWEKA UCHAGUZI MKUU SIMBA, SASA NURU YAANGAZIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top