Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Azam FC kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013-2014 akiwapiku Anthony Matogolo wa Mbeya City na Lugano Mwangama wa Prisons.
Kwa ushindi huo, Kipre amezawadiwa kitita cha Sh. Milioni 5.2.
Aidha, kipa wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hussein Sharrif ‘Cassilas’ ameshinda tuzo ya mlinda mlango bora wa Ligi Kuu akiwapiku David Burhan wa Mbeya City na Beno Kakolanya wa Prisons.
Juma Mwambusi Mwambusi wa Mbeya City, alishinda tuzo kocha bora, akiwaangusha Charles Boniface Mkwasa wa Yanga SC na Mecky Mexime wa Mtibwa Sugar na kupewa Sh. Milioni 5.2.
Refa Israel Mujuni Nkongo wa Dar es Salaam ameibuka mwamuzi bora akilamba Sh. milioni 7.8 baada ya kuwabwaga Isihaka Shirikisho wa Tanga na Jonasia Rukia wa Kagera walioingia kwenye kipengele hicho.
Tuzo ya Mfungaji bora wa msimu ilikwenda kwa mshambuliaji wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe, aliyefunga mabao 19 na kuzawadiwa Sh. Milioni 5.2.

Azam FC wakipokea zawadi ya ubingwa |
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga SC, Salum Rupia akipokea zawadinya ushindi wa pili |
Mweka Hazina wa Azam FC, Karim Mapesa akipokea hundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom, Kevin Tisa |
0 comments:
Post a Comment