KLABU ya Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa Paris St Germain, Ezequiel Lavezzi.
Klabu hiyo ya Ufaransa imemsajili David Luiz na inawataka pia Eden Hazard, Oscar na Petr Cech, wachezaji wengine wa Chelsea pia.
Tayari katika majadiliajo yao inafahamika Chelsea imeuliza bei ya kuuzwa kwa Muargentina Lavezzi ambaye ana nia ya kucheza michuano ya ushindani zaidi.
Atatinga uzi wa bluu? Namna ambavyo Lavezzi ataonekana katika jezi ya Chelsea, kama ambavyo anaonekana kwenye picha hii ya 'kubumba'
Nyota: Lavezzi alifunga dhidi ya Chelsea timu hizo zilipokutana katika Ligi ya Mabingwa msimu huu
Wanafuatia? Klabu hiyo ya Ufaransa inawataka pia Eden Hazard (kushoto) na Oscar (kulia) kutoka Chelsea
Nguzo ya ulinzi: Mourninho anataka kuwapiga bao Manchester City katika kuwania saini ya Mangala baada ya kugundua Varane hawawezi kumpata
Chelsea inasaka mshambuliaji ya Samuel Eto'o kuingizwa katika orodha ya wachezaji wa kutemwa, na inafikiriwa wameelekeza nguvu zao kwa Lavezzi pamoja na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa.
Jose Mourinho pia anamtaka mchezaji ambaye Manchester City pia wanamtaka, kiungo wa ulinzi Eliaquim Mangala wa Porto baada ya kugionga mamba kwa Raphael Varane wa Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment