// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); FRANK DOMAYO: KWA VYOVYOTE, NITAHESHIMU MAKUBALIANO YANGU NA AZAM FC, MIMI NI MKRISTO SAFI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE FRANK DOMAYO: KWA VYOVYOTE, NITAHESHIMU MAKUBALIANO YANGU NA AZAM FC, MIMI NI MKRISTO SAFI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, May 02, 2014

    FRANK DOMAYO: KWA VYOVYOTE, NITAHESHIMU MAKUBALIANO YANGU NA AZAM FC, MIMI NI MKRISTO SAFI

    Na Jackline Charles, Mbeya
    KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Frank Domayo amesema amekwishamalizana na Azam FC na kwa vyovyote ataheshimu makubaliano yake na klabu hiyo kwa kuwa yeye ni Mkristo safi.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana mjini hapa, Domayo amesema kwamba amesaini Mkataba wa miaka miwili na Azam FC na amesikia kashikashi alizozipata kiongozi wa klabu hiyo aliyekuja hapa kumsainisha, lakini kwa vyovyote ataheshimu makubaliano.
    “Nimesikia, lakini ninavyojua hakuna Mkataba uliochanwa, ila hata kama Mkataba umechanwa, mimi nina nakala yangu, na kwa vyovyote nitaheshimu makubaliano, mimi ni Mkristo safi,”alisema.
    Nitaheshimu Mkataba; Frank Domayo kushoto akiwa na meneja wa Azam FC, Jemadari Said kulia baada ya kusaini Mkataba na klabu hiyo juzi mjini hapa


    Hata hivyo, Domayo hakutaka kuzungumza zaidi akisema kwa sasa akili yake anaielekeza kwenye mchezo wa Taifa Stars na Malawi Jumapili mjini hapa.
    “Hayo yamekwishapita kwa upande wangu, kwa sasa akili yangu naielekeza kwenye mchezo wa Malawi,”alisema.
    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana alisema kwamba amemteua Wakili Wilson Ogunde kuchunguza mlolongo mzima wa tukio la usajili wa Domayo juzi mjini hapa.
    Malinzi alisema baada ya kukamilisha uchunguzi wake, Wakili Ogunde ataishauri TFF kuhusu hatua za kisheria na kikanuni za kuchukua. Malinzi ametoa wito kwa wachezaji, klabu na wadau wa mpira wa miguu kufuata kanuni na taratibu katika utendaji wao.
    Viongozi wa Azam FC juzi walikwenda kwenye kambi ya Taifa Stars kukamilisha taratibu za usajili na kiungo Frank Domayo, aliyemaliza Mkataba wake Yanga SC.
    Baada ya kufanikiwa kumsainisha Mkataba wa miaka miwili, wasimamizi wa kambi waliwaitia Polisi viongozi wa Azam FC ambao hata hivyo baadaye waliachiwa. Lakini inadaiwa fomu za usajili zilichanwa.
    Mkristo safi; Frank Domayo amesema ataheshimu makubaliano yake na Azam FC

    Azam si klabu ya kwanza kusajili mchezaji katika kambi ya timu ya taifa, kwani vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga ndiyo waasisi wa mchezo huo.
    Mwaka jana Simba SC walisaini Mkataba mpya na kiungo wao, Amri Kiemba akiwa katika kambi ya Taifa Stars, hoteli ya Tansoma mjini Dar es Salaam.
    Yanga SC iliwasajili Domayo kutoa JKT Ruvu, Kevin Yondan kutoka Simba SC wote wakiwa katika kambi ya Taifa Stars Dar es Salaam miaka miwili iliyopita. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FRANK DOMAYO: KWA VYOVYOTE, NITAHESHIMU MAKUBALIANO YANGU NA AZAM FC, MIMI NI MKRISTO SAFI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top