Na Juma Pinto, LISBON
KOCHA mstaafu, Sir Alex Ferguson jana alimkabidhi tuzo Angel Di Maria ya mchezaji bora wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa kwa kuifunga Atletico Madrid mabao 4-1 Uwanja wa Luz mini hapa.
Gwiji huyo wa Manchester United alitoa mchango mkubwa katika ushindi huo, baada ya Cristiano Ronaldo na Gareth Bale kuzidiwa maarifa na mabeki wa Atletico Madrid.
Tukio hilo lilifuatia saa kadhaa baada ya Ferguson kuuza mvinyo wake kwa Pauni Milioni 2 katika mnada jana.
Nyota wa mchezo: Sir Alex Ferguson akimkabidhi Angel Di Maria tuzo ya mchezaji bora mechi baada ya mchezo jana
Anateleza: Di Maria alikuwa bora zaidi ya mchezaji yeyote wa Real Madrid jana
0 comments:
Post a Comment