KIPA wa kimataifa wa Poland, Lukasz Fabianski amesaini Mkataba wa miaka minne na Swansea baada ya kukubali kuondoka akimaliza Mkataba wake.
Mlinda mango huyo mwenye umri wa miaka 29 atakuwa mchezaji rasmi wa Swansea Julai 1, wakati Mkataba wake utakapomalizika Emirates.
Fabianksi, ambaye ameichezea mechi 21 nchi yake, anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Garry Monk tangu alipotajwa kuwa kocha wa kudumu wa klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment