BEKI Patrice Evra ameongeza Mkataba wa mwaka mmoja Manchester United, klabu hiyo imethibitisha.
Ilionekana kama Evra mwenye umri wa miaka 33 ataondoka baada ya United kuweka mezani dau la Pauni Milioni 27 kumnunua beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw.
Lakini beki huyo aliyetua United mwaka 2006 akitokea Monaco ya nyumbani kwao, Ufaransa ameamua kuendelea na kazi hadi mwisho wa mwaka wa kwanza wa Louis van Gaal kazini.
0 comments:
Post a Comment