UBAGUZI wa rangi umezidi Hispania, baada ya mchezaji wa Levante, Pape Diop kuzomewa na kufanyiwa ishara za nyani jana na mashabiki wa Atletico Madrid wakati wa mechi ya La Liga.
Wiki moja baada ya beki wa Barcelona, Dani Alves alipolazimika kula ndizi aliyotupiwa na mashabiki, kiungo huyo wa Senegal alisema alicheza kama nyani mbele ya waliomzomea na kumkebehi.
"Waliniita nyani,niligeukia na kujifanya nyani," alisema Diop na kukaririwa na Marca.com. "Nimechoka na ubaguzi katika soka. Na upo mwingi.
"Nilicheza kama nyani kuliainisha tatizo. Nilitaka watu wajue kilichotokea. Sijui kama ni ubaguzi, au kudharauliana, lakini wanatakiwa kuacha ishara za nyani wanazowafanyia watu,"alisema.'
Alves alipata sapoti kubwa kutoka kwa wachezaji wake na Rais wa FIFA, Sepp Blatter baada ya tukio lilitokea katika mechi na Villarreal wiki iliyopita.
Mashabiki wa Atletico jana waliondoka wanyonge baada ya bao la kujifunga la Filipe Luis na lingine la David Barral kuopunguza matumaini yao ya kutwaa ubingwa wa La Liga baadaye mwezi huu
Kazi kazi: Diop (kulia) akiteleza miguuni mwa Toby Alderweireld wa Atletico kuondosha mpira jana Levante ikishinda 2-0
Wanyonge: Wachezaji wa Atletico kutoka kushoto Filipe Luis, Thibaut Courtois na Adrian Lopez wakiondoka kinyinge baada ya mechi jana
0 comments:
Post a Comment