BEKI David Luiz amefaulu vipimo vya afya na kukubaliana juu ya Mkataba na Paris Saint-Germain kuelekea uhamisho wa Pauni Milioni 50 kuhamia kwa wababe hao wa Ufaransa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kuwa beki ghali duniani uhamisho wake ukipiku usajili wa mabeki wawili waliokuwa wanashikilia rekodi ya wachezaji ghali wa nafasi ya ulinzi waliponunuliwa na PSG, Marquinhos na Thiago Silva.
Wawakilishi wa PSG leo walisafiri hadi Brazil kwenda kukamilisha vipimo vya mchezaji huyo aliye kambini na timu ya wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment