Hakuna tatizo kabisa: Mwanasoka Bora wa Dunia Cristiano Ronaldo akifanya mazoezi na timu yake, Real Madrid leo kujiandaa na mchezo wa kesho wa Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Luz mjini Lisbon, Ureno dhidi ya jirani zao, Atletico Madrid. Kocha wa Real, Carlo Ancelotti ana matumaini mchezaji huyo atakuwa fiti kwa asilimia 100 kesho.
Ronaldo na wachezaji wenzake wanaonekana wapo tayari kabisa kubeba taji la 10 la Ligi ya Mabingwa kesho
Ronaldo akitaniana na gwiji wa Real Madrid, Raul (kushoto) na kipa Iker Casillas
Beki Pepe akipatiwa huduma ya kwanza mazoezini leo Lisbon
Karim Benzema kulia akipiga danadana
0 comments:
Post a Comment