Na Reatus Mahima, Mbeya
NAHODHA wa timu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amepewa shavujingine na kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mholanzi Mart Nooij baada ya kupewa mikoba ya kuwa nahodha wa timu hiyo.
Cannavaro ambaye ni beki wa kati amechukua mikoba ya beki mwenzake wa Yanga, Kevin Yondani aliyetimuliwa kambini na Nooij baada ya kutoripoti kambini wakati Stars ikijiandaa na mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi iliyoisha kwa Stars kufungwa mabao 3-0. Hata hivyo, Yondani alirudishwa kambini jijini hapa juzi.
Cannavaro alianza kushika madaraka hayo katika mechi ya juzi ya Stars iliyocheza na Malawi na timu hizo kwenda suluhu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini hapa.
Aidha Nooij amemteua beki mwenzie wa kati anayechezea timu ya Azam FC, Aggrey Morris kuwa nahodha msaidizi wa timu hiyo.
Awali kwenye mechi ya Burundi, Morris ndiye alivaa kitambaa cha unahodha, lakini baada ya Cannavaro kuongezwa Stars baada ya mechi hiyo Nooij alimpa majukumu hayo.
“Nachukulia changamoto kocha kuniteua kama nahodha. Tulijitahidi kupambana dhidi ya Malawi lakini kwenye mpira kuna matokeo matatu, kushinda kufungwa na sare, tutajipanga vyema kushinda mechi yetu dhidi ya Zimbabwe, ambayo ni muhimu kwetu,” alisema Cannavaro akizungumzia mechi dhidi ya Malawi akiwa kama nahodha.

Nadir Haroub 'Cannavaro' amepewa Unahodha wa Taifa Stars |

0 comments:
Post a Comment