// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CAF YAIFUNGIA GAMBIA MIAKA MIWILI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA AFRIKA, KISA KUTUMIA VIJEBA MICHUANO YA VIJANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CAF YAIFUNGIA GAMBIA MIAKA MIWILI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA AFRIKA, KISA KUTUMIA VIJEBA MICHUANO YA VIJANA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, May 03, 2014

    CAF YAIFUNGIA GAMBIA MIAKA MIWILI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA AFRIKA, KISA KUTUMIA VIJEBA MICHUANO YA VIJANA

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    KAMATI Kuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) chini ya Rais wake, Issa Hayatou ilikutana Aprili 29 na 30 mwaka huu makao makuu mjini Cairo, Misri na kuifungia Gambia katika mashindano yake yote kwa miaka miwili kutokana na udanganyifu wa umri wa wachezaji.
    Taarifa ya CAF iliyotumwa BIN ZUBEIRY leo, imesema Kamati Kuu imekifungia Chama cha Soka Gambia kwa miaka miwili kutoshiriki mashindano yake yote kwa mujibu wa Ibara ya 37, aya ya kwanza ya kanuni za mashindano ya U-20, ambayo inasema yeyote atakayehusika na udanganyifu atafungiwa kwa miaka miwili kutoshiriki michuano yote ya shirikisho hilo.
    Rais wa CAF, Issa Hayatou kulia akiwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi kushoto

    Aprili 20, mwaka huu Kamati ya Maandalizi ya michuano ya U-20 iliamua kuiondoa mashindanoni Gambia kuwa kuchomekea wachezaji watano waliozidi umri katika mchezo wa kufuzu dhidi ya Liberia Aprili 6, 2014. 
    Wachezaji wote watano walizaliwa mwaka 1994 wakati mashindano hayo yaliyoanza Septemba 2 mwaka jana, yako wazi kwa vijana waliozaliwa kuanzia  Januari 1, mwaka 1995.
    Pamoja na hayo, CAF imeanzisha uchunguzi wa kesi ya mchezaji Ali Sowe, aliyeripotiwa kuzaliwa Juni 14 mwaka 1994 akitumia paspoti namba 332465 ambaye ni miongoni mwa wachezaji watano walioiponza Gambia kufungiwa, kwani tayari mchezaji huyo amekwishawahi kusajiliwa CAF mwaka 2012 na klabu ya Gamtel FC iliyoshiriki Kombe la Shirikisho kwa jina lile na namba ile ile, lakini tarehe tofauti ya kuzaliwa Oktoba 14,mwaka 1988.
    Jumla ya masuala 15 yalikuwa ajenda kwenye kikao hicho, ikiwemo kanuni za Kombe la Mataifa ya Afrika, michuano ya klabu na kanuni za adhabu, ambayo kila moja lilijadiliwa kwa kina na Kamati hiyo.
    Kamati Kuu ilipitia taarifa mbalimbali kutoka makundi mbalimbali yaliyopewa majukumu ya kusimamia shughuli za shirikisho hilo katika siku hizo mbili, lakini ikaachia nafasi ya masuala ya kikao kijacho cha Juni 8, 2014 mjini Sao Paulo, Brazil.
    Pamoja na hayo kikao kilipitia taarifa zilizokiuka maagizo yake ya kikao cha Januari juu ya kanuni za mashindano yote ya CAF, ambayo yanasema nchi yoyote ambayo klabu yake au timu ya taifa itahusishwa na uvunjaji wa sheria za haki za CAF mara moja itaondolewa kwenye michuano yote ifuatayo ya shirikisho hilo.
    Ilipitia taarifa za mashindano yote yaliyopita yakiwemo Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake nchini Namibia 2014; Michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Niger mwakani, michuano ya U-20 Senegal mwakani pia na Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
    Kamati Kuu imeamua kurudisha nyuma mashindano ya U-17 nchini Niger mwakani kutoka Mei 2 na 16 hadi Februari 15 na Machi 1 mwaka 2015 kuhakikisha vijana wadogo wanashindana katika hali ya hewa nzuri.
    Mashindano ya kwanza ya soka ya ufukweni Afrika yatafanyika kuanzia Aprili 14 hadi 19 mwaka 2015 nchini Shelisheli wakati michuano ya pili ya U-23 itafanyika kadi ya Desemba  5 na 19 mwakani DRC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YAIFUNGIA GAMBIA MIAKA MIWILI KUSHIRIKI MASHINDANO YOYOTE YA AFRIKA, KISA KUTUMIA VIJEBA MICHUANO YA VIJANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top