KOCHA Brendan Rodgers amevuna matunda ya kazi yake nzuri Liverpool baada ya kusainishwa Mkataba mpya ambao utamuweka Anfield kwa muda mrefu.
Rodgers, aliyekuwa amebakiza miezi 12 na nafasi ya kuongezewa mwaka mmoja katika mkataba wake, amesaini mkataba mpya ambao utamuweka Merseyside hadi mwaka 2018.
Liverpool ilizidiwa kwa point mbili tu na Manchester City walioibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya England, hiyo ikiwa mara ya kwanza kufika hatua hiyo tangu mwaka 1990 tena ikiwavutia wengi msimu huu kwa soka maridadi ya kisasa inayofundishwa na Rodgers.
Wamiliki wa klabu hiyo, Fenway Sports Group kutoka Marekani, wamevutiwa na kazi ya mwalimu huyo waliyemuajiri kutoka Swansea Juni mwaka 2012 na kuamua kumtia pingu.
REKODI YA BRENDAN RODGERS LIVERPOOL
Mechi 97 Ameshinda 54 Sare 21 Amefungwa 22
Amefunga mabao 206 Amefungwa mabao 118 (+88)
Asilimia ya ushindi 55.67
Amefunga mabao 206 Amefungwa mabao 118 (+88)
Asilimia ya ushindi 55.67
Mmiliki wa klabu John Henry na Mwenyekiti, Tom Werner kwa pamoja wamesema: "Tuna bahati sana kuwa na kipaji hiki kikubwa cha kipekee kuongoza soka yeti na ambaye juu yake tunaamini ataleta mafanikio zaidi katika harakati zebu za pamoja na kuiendeleza klabu ya Liverpool.
"Brendan anatutia moyo, kama wamiliki, tunaojaribu kutafuta mafanikio ya uwanjani. Msimu huu amefufua matumaini ya kila mmoja kwamba tunaweza muleta mafanikio Liverpool na wote tunajifunga kufanya kazi pamoja kusaka hayo mafanikio,".
0 comments:
Post a Comment