• HABARI MPYA

    Friday, May 23, 2014

    BLATTER AKUNWA NA MIPANGO YA MALINZI TFF

    Na Boniface Wambura, DAR ES SALAAM
    Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter amefurahishwa na mipango ya maendeleo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kuahidi kusaidia miradi mbalimbali.
    Blatter alisema hayo jana (Mei 22 mwaka huu) ofisini kwake jijini Zurich, Uswisi baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
    Blatter kushoto akiwa na Malinzi


    FIFA itaisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo kama Goal, lakini pia itasaidia kutoa mafunzo kwa makocha, waamuzi wa mpira wa miguu, madaktari wa tiba ya michezo na watawala.
    Vilevile shirikisho hilo la kimataifa lililoanzishwa mwaka 1904 litasaidia katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu mbalimbali ya mpira wa miguu nchini Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BLATTER AKUNWA NA MIPANGO YA MALINZI TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top