LICHA ya kucheza pungufu ya mchezaji mmoja, Benfica ya Ureno imerudi kwenye fainali ya Europa League kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kutoka sare ya 0-0 na Juventus jana hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1.
Juventus ilitengeneza nafasi nyingi nzuri, lakini ikashindwa tu kumtungua kipa wa Benfica, Jan Oblak, ambaye aliokoa michomo mingi ya hatari.
Licha ya Benfica kumpoteza mchezaji mmoja dakika ya 67 baada ya refa wa England, Mark Clattenburg kumpa kadi ya pili ya njano kiungo Muargentina, Enzo Perez kwa kumchezea rafu Arturo Vidal, kikosi cha Jorge Jesus kilimudu mchezo. Benfica itakutana na Sevilla ambayo jana nayo imeitoa Valencia, zote za Hispania kwa kuifunga mabao 2-0 na kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini baada ya awali kufungwa 3-1 katika mchezo wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment