KLABU ya Barcelona imeteua Nahodha wake wa zamani, Carles Puyol, ambaye maisha yake ya uwanjani yamekatishwa na maumivu ya goti mwishoni mwa msimu ukiopita kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mchezo, chinu ya Andoni Zubizarreta.
"Nataka kuwashukuru FC Barcelona kwa kila kitu walichonipa kabla na kwa kunioa nafasi hii sasa," amesema Puyol, ambaye ataanza majukumu yake mapya Septemba.
Majukumu mapya: Carles Puyol (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo kuanzia Septemba
Puyol aliwaaga wapenzi wa Barca katika Mkutano maalum na Waandishi wa Habari mwezi huu baada ya kushinda mataji 21 akiwa na klabu hiyo.
Beki huyo mfuga minywele, aliyeshinda Kombe la Dunia, la ubingwa wa Mataifa ya Ulaya akiwa na Hispania ba ambaye alikuwa kivutio kwa staili yake ya uchezaji ya kujituja bila kukata tamaa, alianza kuichezea Barca chini ya kocha wa zamani Louis van Gaal na akaisaidia kushinda mataji ya Ligi ya Mabingwa miaka ya 2006, 2009 na 2011.
Alikuwa sehemu ya kikosi cha Pep Guardiola kilichobeba mataji sita mwaka 2009 ambacho kilishinda mataji tote kilichoshindania mwaka huo, lakini kutokana na majeruhi msimu uliopita alicheza mechi tano tu za La Liga.
Gwiji: Puyol alishinda mataji 21 enzi zake Nou Camp kabla ya kulazimika kustaafu kwa sababu ya majeruhi
0 comments:
Post a Comment