Na Prince Akbar, Dar es Salaam
HIMID Mao Mkami anaweza kuwa mchezaji mwenye viatu vingi zaidi vya kuchezea soka nchini- hadi sasa akiwa ana jozi 16.
Kiungo huyo wa Azam FC anayeweza kucheza kama beki pia, amesema kwamba anaithamini sana kazi yake na kuipenda pia, ndiyo maana vifaa vya kazi anavyo vingi.
“Siri ya mafanikio ni kukipenda unachokifanya kwa moyo wako mmoja na si kwa sababu unapata kitu fulani kupitia kazi yako au hicho kitu. Naipenda kazi yangu,”alisema mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Pamba SC ya Mwanza, Mao Mkami ‘Ball Dancer’.
Himid mbali na viatu, kila kitu kinachohusiana na kazi yake- kuanzia jezi vizuia ugoko na kadhalika anavyo vya kutosha.
Himid sasa anaonekana kuwaambukiza tabia hiyo na wachezaji wenzake wa Azam FC ambao nao wameanza kukusanya vifaa vingi vya mchezo.
“John Bocco naye ananiiga sasa, ameanza kukusanya zana za kazi na wachezaji wengine pia wamevutiwa na kile ninachokifanya nao wameamua kufanya kama mimi,”amesema.
Msimu huu Himid anaweza kutimiza ndoto zake za kutwaa taji la kwanza la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara akiwa na Azam FC kutokana na hadi sasa kuongoza ligi hiyo ikiwa imefika ukingoni.
Pazia la Ligi Kuu likiwa linafungwa Aprili 19, mwaka huu, Azam FC ina pointi 53 ilizovuna katika mechi 23, Yanga SC pointi 46 ilizovuna kwenye mechi 22 na Mbeya City ina pointi 45 za mechi 23, ingawa leo inacheza na Ashanti United.

Naipenda kazi yangu; Himid Mao na viatu vyake, nani mwingine anavyo vingi? |

0 comments:
Post a Comment