Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
YANGA SC imezinduka na kufufua matumani ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kutimiza pointi 49 baada ya kucheza mechi 23 sawa na Azam FC inayoongoza ligi hiyo kwa pointi zake 53. Mbeya City ni ya tatu kwa pointi zake 46 baada ya kucheza mechi 24.
Yanga leo ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0, Mrisho Ngassa akifunga la kwanza dakika ya tisa akimalizia pasi nzuri ya Mrundi Didier Kavumbangu ndani ya boksi.
Ngassa tena akafunga bao lake la 11 katika Ligi Kuu msimu huu dakika ya 15 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Shaaban Dihile kufuatia shuti kali la Kavumbangu aliyepokea pasi ya Simon Msuva.
Ukawadia wakati wa Kavumbangu kufunga mwenyewe dakika ya 41 akiitendea haki pasi nzuri ya mtaalamu Mrisho Khalfan Ngassa.
Kipindi cha pili Yanga SC, Yanga ilirudi na moto wake na dakika ya 48, Ngassa akatimiza hat trick, hiyo ikiwa ni ya kwanza msimu huu wa ligi kwa shuti la umbali wa takriban mita 20.
Hussein Javu aliyeingia kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza alifunga bao la tano dakika ya 53.
Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga, Freddy Felix Minziro lilifungwa na Iddi Mbaga dakika ya 83 akimalizia krosi ya Damas Makwaya.
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Frank Domayo, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Didier Kavumbangu, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Hussein Javu dk45.
JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Damas Makwaya, Edward Charles, Omar Mtaki, Jamal Machelanga, Nashon Naftal, Sino Augustino, Emmanuel Swita/Haroun Adolph dk36, Iddi Mbaga, Hussein Bunu/Amos Mgisa dk50 na Karage Gunda.
YANGA SC imezinduka na kufufua matumani ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii.
Ushindi huo, unaifanya Yanga SC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm kutimiza pointi 49 baada ya kucheza mechi 23 sawa na Azam FC inayoongoza ligi hiyo kwa pointi zake 53. Mbeya City ni ya tatu kwa pointi zake 46 baada ya kucheza mechi 24.
Mfungaji wa mabao matatu ya Yanga katika ushindi wa 5-1 dhidi ya JKT Ruvu, Mrisho Ngassa wa pili kulia akisha ngilia na wenzake jioni hii Uwanja wa Taifa |
Ngassa tena akafunga bao lake la 11 katika Ligi Kuu msimu huu dakika ya 15 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Shaaban Dihile kufuatia shuti kali la Kavumbangu aliyepokea pasi ya Simon Msuva.
Ukawadia wakati wa Kavumbangu kufunga mwenyewe dakika ya 41 akiitendea haki pasi nzuri ya mtaalamu Mrisho Khalfan Ngassa.
Kipindi cha pili Yanga SC, Yanga ilirudi na moto wake na dakika ya 48, Ngassa akatimiza hat trick, hiyo ikiwa ni ya kwanza msimu huu wa ligi kwa shuti la umbali wa takriban mita 20.
Hussein Javu aliyeingia kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza alifunga bao la tano dakika ya 53.
Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu inayofundishwa na kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga, Freddy Felix Minziro lilifungwa na Iddi Mbaga dakika ya 83 akimalizia krosi ya Damas Makwaya.
Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Frank Domayo, Simon Msuva, Hassan Dilunga, Didier Kavumbangu, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Hussein Javu dk45.
JKT Ruvu; Shaaban Dihile, Damas Makwaya, Edward Charles, Omar Mtaki, Jamal Machelanga, Nashon Naftal, Sino Augustino, Emmanuel Swita/Haroun Adolph dk36, Iddi Mbaga, Hussein Bunu/Amos Mgisa dk50 na Karage Gunda.
0 comments:
Post a Comment