Na Dina Ismail, Dar es Salaam
KIKOSI cha Yanga SC kipo njiani kurejea Dar es Salaam, kikitokea Moshi mkoani Kilimanjaro ambako jana kilicheza mechi ya kirafiki kikitokea Arusha katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Oljoro.
Yanga iliyoifunga Panone ya Kilimanjaro mabao 3-0 jana wafungaji Didier Kavumbangu, Mrisho Ngassa na Hussein Javu inaweza kuingia kambini katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani leo kujiandaa na mchezo dhidi ya mahasimu, Simba SC Jumamosi.
Mchezo huo wa kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, unakuja wakati bingwa amekwishapatikana ambaye ni Azam FC na mshindi wa pili kadhalika, ambaye ni Yanga.
Mchezo wa Jumamosi ni muhimu kwa Yanga SC kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-1 na Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Desemba 21, mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipigo cha Desemba kiliifanya Yanga SC ikavunja benchi lake zima la Ufundi kwa kuwafukuza makocha Mholanzi, Ernie Brandts na Wasaidizi wake Freddy Felix Minziro na Razack Ssiwa, ikiwaajiri Mholanzi mwingine, Hans van der Pluijm, Charles Boniface Mkwasa na Juma Nassor Pondamali.
Benchi jipya la Ufundi Yanga SC baada ya kuikosesha timu ubingwa, sasa linakabiliwa na mtihani mwingine wa kurejesha heshima mbele ya watani wao, Simba SC Jumamosi.

0 comments:
Post a Comment