TIMU ya Valencia ya Hispania imetinga Nusu Fainali ya Europa League kufuatia kuifunga Basle ya Uswisi mabao 5-0.
Timu ya Uswisi ilishinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza nyumbani, lakini Valencia imeweza kupanda mlima shukrani kwake, Paco Alcacer aliyepiga hat-trick.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka nyuma kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza na kusonga mbele tangu Europa League ilipofanyika kwa mara ya kwanza msimu wa 2009-2010.
Shujaa: Mabao matatu ya Paco Alcacer yalitoa mchango mkubwa jana Valencia kutinga Nusu Fainali
Mbali na mabao ya Alcacer, Eduardo Vargas na Juan Bernat walifunga mabao mengine kukamilisha ushindi wa kihistoria.
Basle ilijikuta dhaifu zaidi uwanjani baada ya kupoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu, Marcelo Diaz na Gaston Sauro.
Juventus ya Italia nayo imesonga mbele kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Lyon ya Ufaransa.
Andrea Pirlo akiifungia kwa mpira wa adhabu Juventus
Mfungaji wa bao la ushindi la Juventus, Claudio Marchisio akishangilia
Watalianlo hao walishinda 1-0 katika mchezo wa kwanza na wakapata bao la pili jana dakika ya nne tu ya mchezo huo, kwa shuti la mpira wa adhabu la Andrea Pirlo.
Jimmy Briand aliifungia Lyon bao la ugenini dakika ya 18, lakini Claudio Marchisio akaifungia bao la pili Juventusdakika ya 68.
Sevilla pia imetinga Nusu Fainali baada ya kuitoa Porto ya Ureno kwa mabao 4-2 jumla. Porto iliifunga Sevilla 1-0 katika mchezo wa kwanza, lakini timu hiyo ya Hispania jana imejibu mapigo kwa ushindi wa 4-1.
Carlos Bacca aliifungia Sevilla jana
Ivan Rakitic alifunga bao la kwanza kwa penalty dakika ya tano baada ya Carlos Bacca kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari.
Vitolo aliifungia Sevilla bao la pili dakika ya 26 na Bacca akafunga la tatu dakika tatu baadaye.
Wachezaji wa Sevilla wakishangilia
La pili: Rodrigo amefunga mabao mawili Benfica ikiibwaga AZ Alkmaar
Kipindi cha pili Sevilla ilipata pigo baada ya Coke kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 54, lakini bado hiyo haikuwasaidia Porto na Kevin Gameiro akafunga la nne dakika ya 79.
Ricardo Quaresma aliifungia Porto bao la kufutia machozi dakika za majeruhi.
Kutakuwa na mwakilishi mwingine wa Ureno baada ya Benfica kuifunga 2-0 AZ Alkmaar, na kufanya ushindi wa jumla wa 3-0, shukrani kwake Rodrigo aliyefunga kila kipindi.
0 comments:
Post a Comment