// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAZITHIBITISHA NDANDA, STAND UNITED NA POLISI MORO KUPANDA LIGI KUU, PAMBA YAPOROMOKA HADI LIGI YA MKOA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAZITHIBITISHA NDANDA, STAND UNITED NA POLISI MORO KUPANDA LIGI KUU, PAMBA YAPOROMOKA HADI LIGI YA MKOA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 08, 2014

    TFF YAZITHIBITISHA NDANDA, STAND UNITED NA POLISI MORO KUPANDA LIGI KUU, PAMBA YAPOROMOKA HADI LIGI YA MKOA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezithibitisha timu za Ndanda SC ya Mtwara, Polisi ya Morogoro na Stand United ya Shinyanga kupanda daraja kutoka la Kwanza, kwenda Ligi Kuu ya Vodacom msimu ujao.
    Taarifa ya TFF kwa BIN ZUBEIRY leo, imesema timu tatu za Ligi Daraja la Kwanza zitacheza Ligi ya Mkoa katika mikoa yao msimu ujao baada ya kushika nafasi za mwisho katika makundi yao, hivyo kushuka daraja.
    Prisons inaweza kuwa moja ya timu zitakazoshuka Daraja kuzipisha Ndanda, Polisi na Stand United

    Transit Camp imeshika nafasi ya mwisho katika A wakati Mkamba Rangers imeshuka daraja kwa kukamata mkia katika kundi B. Nayo Pamba SC imerudi kucheza Ligi ya Mkoa wa Mwanza baada ya kuwa ya mwisho kwenye kundi C.
    Timu zilizopanda daraja kutoka FDL kwenda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao ni Ndanda SC ya Mtwara kutoka kundi A, Polisi Morogoro ya kundi B na Stand United ya Shinyanga iliyoibuka kinara katika kundi C.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAZITHIBITISHA NDANDA, STAND UNITED NA POLISI MORO KUPANDA LIGI KUU, PAMBA YAPOROMOKA HADI LIGI YA MKOA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top