Na Dina Ismail, Dar es Salaam
KITENDO cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kukifuta kipengele kipya cha 26 cha Katiba mpya ya Simba SC na kurejesha kipengele cha zamani, ni kinyume cha ushauri wa kitaalamu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, BIN ZUBEIRY imebaini.
TFF ilidai pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu sifa za mgombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF, ikaagiza kipengele cha zamani kibaki vilevile bila kubadilishwa.
Lakini habari za kiuchunguzi, ambazo BIN ZUBEIRY imezipata ni kwamba, TFF ilimuandikia barua Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kuomba ufafanuzi juu ya kipengele hicho.
Hatua hiyo ya TFF ilifuatia barua waliyoandikiwa na wanachama wao, Chama cha Soka Pwani (COREFA) ikipinga kipengele 29 (4) cha Katiba ya TFF.
Barua ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwenda TFF imeunga mkono ombi la COREFA na kusistiza kuwa kipengele hicho ni kinyume cha utangulizi wa Katiba yao wenyewe TFF, CAF, FIFA na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba kumbagua au kumtenga yeyote ni makosa, hivyo itabidi Msajili wa Vyama vya Michezo ahakikishe Katiba zote za klabu na vyama hazipingani na Katiba ya nchi.
Maana yake- hata TFF pia watalazimika kufanyia marekebisho Katiba yao, juu ya kipengele hicho kinachopingana na Katiba ya nchi kwa mujibu wa barua ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa ushauri huo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali- ina maana baada ya TFF kukiondoa kipengele kipya cha 26 cha Katiba ya Simba SC, inaweza kukwama kupitishwa na Msajili wa Vyama na klabu za Michezo nchini.
Juhudi za kumpata Rais wa TFF, Jamal Malinzi kuzungumzia suala hilo hazikufanikiwa kwa kuwa bado yupo Afrika Kusini kwenye semina ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), pamoja na Katibu wake, Celestine Mwesigwa na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi.
TFF iliagiza mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Simba uendelee kama ulivyopangwa wakizingatia uamuzi huo, wakati huo huo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji iliishauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo kugombea.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema |

0 comments:
Post a Comment