// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAIPONGEZA TIMU YA WATOTO WA MITAANI KUTWAA UBINGWA WA DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAIPONGEZA TIMU YA WATOTO WA MITAANI KUTWAA UBINGWA WA DUNIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 07, 2014

    TFF YAIPONGEZA TIMU YA WATOTO WA MITAANI KUTWAA UBINGWA WA DUNIA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeipongeza timu ya Tanzania ya Watoto wa Mitaani kwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
    TFF imesema ushindi wa timu hiyo ni fahari kwa Tanzania, lakini kubwa ni kwa kituo cha Mwanza ambacho ndicho kinachoiendesha pamoja na wadhamini na wafadhili walioiwezesha kushiriki fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo.

    “Vilevile ushindi huo unatoa changamoto kubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kuwa watoto wa mitaani ni sehemu tu ya vipaji vilivyotapaa nchini, hivyo iliyopo ni kuvisaka na kuvibaini vipaji hivyo kwa ajili ya ustawi wa mchezo huo nchini,” imesema taarifa ya TFF.
    TFF imeahidi kuendelea kushirikiana na kituo hicho cha Mwanza, na vingine vyote ambavyo vinajishughulisha na mchezo huu, lengo likiwa ni kuundeleza na hata kutoa ajira kwa vijana hapo baadaye kupitia mpira wa miguu.
    Timu hiyo inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAIPONGEZA TIMU YA WATOTO WA MITAANI KUTWAA UBINGWA WA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top