// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA, ASHANTI UTD KUVAANA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA, ASHANTI UTD KUVAANA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, April 11, 2014

    SIMBA, ASHANTI UTD KUVAANA TAIFA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea keshokutwa (Aprili 12 mwaka huu)  katika raundi ya 25 ambapo Simba na Ashanti United zitapambana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
    Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya) wakati Coastal Union itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
    Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya wenyeji Oljoro JKT na Yanga.

    Mtibwa Sugar itacheza na Ruvu Shooting (Uwanja wa Manungu, Morogoro), Mgambo Shooting na Kagera Sugar zitaoneshana kazi kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mbeya City ikiumana na Azam kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
    Wakati huo huo: Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali imetambulishwa leo (Aprili 11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
    Baadaye timu hiyo leo itapata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda. Saa 10 jioni itatembeza kombe hilo katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi.
    Jioni imeandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara.
    Katika hatua nyingine Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeteua mwamuzi msaidizi wa Tanzania anayetambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ferdinand Chacha ameteuliwa kuchezesha michezo ya Vijana ya Afrika (AYG- African Youth Games).
    Michezo hiyo ya kwanza ya Afrika itachezesha jijini Gaborone, Botswana kuanzia Mei 22-31 mwaka huu. Tanzania pia itashiriki katika mashindano hayo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15.
    Naye Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga atakuwa na mkutano na waandishi wa habari Jumatatu (Aprili 14 mwaka huu).
    Mkutano huo utafanyika kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zilizopo Ghorofa ya 3, Jengo la PPF Tower mtaa wa Ohio/Garden Avenue kuanzia saa 5 kamili asubuhi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, ASHANTI UTD KUVAANA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top