// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); RUVU SHOOTING INAFUNGWA KOTE, LAKINI SI MABATINI, AZAM FC WANALIJUA HILO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE RUVU SHOOTING INAFUNGWA KOTE, LAKINI SI MABATINI, AZAM FC WANALIJUA HILO? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 08, 2014

    RUVU SHOOTING INAFUNGWA KOTE, LAKINI SI MABATINI, AZAM FC WANALIJUA HILO?

    Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
    KIKOSI cha Azam FC kinachowakosa nyota wake kadhaa kesho kitakuwa na kibarua kigumu mbele ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, uwanja ambao 'maafande' hao hawajapoteza hata mechi moja tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Meneja wa Azam FC, Jemadari Said alisema jana kuwa kikosi chao kitakosa huduma za Samih Nuhu, Joseph Kimwaga, Ismail Gambo, Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote ni majeruhi kwa muda mrefu sasa pamoja na mchezaji wao chipukizi Bryson Raphael aliyerejea jana akichechemea kwa maumivu ya kifundo cha mguu kutoka Kenya alikokwenda kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes).











    TAKWIMU ZA RUVU SHOOTING MSIMU HUU UWANJA WA MABATINI

    MZUNGUKO WA KWANZA
    Ruvu Shooting 3- Prisons (Agosti 24, 2013)
    Ruvu Shooting 1-0 Mgambo (Sept 14, 2013)
    Ruvu Shooting 1-0 JKT Ruvu (Sept 18, 2013)
    Ruvu Shooting 1-0 Rhino (Okt 13, 2013)
    Ruvu Shooting 1-1 Kagera (Okt 28, 2013)
    Ruvu Shooting 2-2 Mtibwa (Nov 3, 2013)

    UWANJA WA TAIFA
    Ruvu Shooting 1-1 Simba (Okt 5, 2013)

    MECHI ZA UGENINI
    Mbeya City 2-1 Ruvu Shooting (Agosti 28, 2013)
    Coastal 1-0 Ruvu Shooting (Sept 22, 2013)
    Yanga 1-0 Ruvu Shooting (Sept 28, 2013)
    Oljoro 2-2 Ruvu Shooting (Okt 9, 2013)
    Ashanti 2-2 Ruvu Shooting (Okt 19, 2013)
    Azam FC 3-0 Ruvu Shooting (Okt 30, 2013)

    MZUNGUKO WA PILI
    Ruvu Shooting 1-1 Mbeya City (Jan 29, 2014)
    Ruvu Shooting 1-0 Coastal (Febr 15, 2014)
    Ruvu Shooting 1-0 Oljoro (Machi 8, 2014)
    Ruvu Shooting 2-0 Ashanti (Machi 22, 2014)

    UWANJA WA TAIFA
    Ruvu Shooting 0-7 Yanga (Febr 22, 2014)

    MECHI ZA UGENINI
    Mgambo 0-0 Ruvu Shooting (Febr 5, 2014)
    Prisons 3-1 Ruvu Shooting (Febr 8, 2014)
    JKT Ruvu 0-2 Ruvu Shooting (Febr 12, 2014)
    Simba 3-2 Ruvu Shooting (Machi 2, 2014)
    Kagera 0-0 Ruvu Shooting (Machi 30, 2014)

    Kikosi cha Thom Olaba cha Ruvu Shooting licha ya kuwa na rekodi mbaya ya kufungwa magoli 7-0 dhidi ya Yanga msimu huu na kushinda mechi moja tu ugenini, kimecheza mechi 10 msimu huu kwenye Uwanja wa Mabatini bila kupoteza hata mechi moja kikishinda nne na sare mbili mzunguko wa kwanza na kushinda tatu na sare moja mzunguko wa pili.
    Masau Bwire, msemaji wa Ruvu Shooting ameiambia BIN ZUBEIRY kwa simu leo mchana akiwa Pwani kuwa benchi lao la ufundi limeiandaa vizuri timu kuhakikisha inalinda heshima ya kutofungwa kwenhye uwanja wa nyumbani na kuwa timu ya kwanza kuifunga Azam FC msimu huu.
    Lakini, kikosi cha Azam FC kinachonolewa na Mcameroon Joseph Omog kimeonekana kuwa tishio zaidi msimu huu kikiongoza ligi kwa pointi nne mbele ya Yanga wanaokamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 46, kilikuwa cha kwanza kuvunja mwiko wa kuifunga Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani mzunguko wa pili huku Simba na Yanga wakichezea vichapo kwenye uwanja huo.
    Azam FC inahitaji ushindi katika mechi hiyo ya raundi ya 24 ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa mara ya kwanza tangu ipande Ligi Kuu 2007 kwani itakuwa pia na kibarua kigumu dhidi ya Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mwishoni mwa wiki. 
    Mbeya City haijapoteza hata mechi moja kwenye uwanja huo tangu kuanza kwa msimu huu Agosti 24 mwaka jana. Azam wataingia uwanjani kesho wakiwa na kumbukumbu ya kuifunga 3-0 Ruvu Shooting katika mechi yao ya mzunguko wa kwanza iliyopigwa Uwanja wa Azam Oktoba 30 mwaka jana.
    Ruvu Shooting inakamata nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 34 ilizozipta katika mechi 23, ikishinda mechi tisa, sare saba na kupoteza saba. Nafasi ya tano inakaliwa na Kagera Sugar wenye pointi 34 pia, tatu nyuma ya Simba katika nafasi ya nne, na 12 nyuma ya Mbeya City walioko nafasi ya tatu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RUVU SHOOTING INAFUNGWA KOTE, LAKINI SI MABATINI, AZAM FC WANALIJUA HILO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top