// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PIGO LINGINE AZAM FC IKIENDA KUIVAA RUVU SHOOTING UWANJA WA MABATINI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PIGO LINGINE AZAM FC IKIENDA KUIVAA RUVU SHOOTING UWANJA WA MABATINI KESHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 08, 2014

    PIGO LINGINE AZAM FC IKIENDA KUIVAA RUVU SHOOTING UWANJA WA MABATINI KESHO

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    AZAM FC itamkosa mchezaji wake chipukizi anayeinukia vizuri, Bryson Raphael katika mchezo wake wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
    Tovuti ya Azam FC imemnukuu Meneja wa klabu hiyo, Jemadari Said Kazumari akisema mchezaji huyo amerejea kutoka Kenya alipokwenda kuichezea timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes akiwa anachechemea kwa maumivu ya kifundo cha mguu.
    Bryson Raphael kushoto akiwa na Aishi Manula kulia, wote wa Azam na Ngorongoro

    Jemadari amesema hilo ni pigo kwa timu kwa sababu huyo ni miongoni mwa wachezaji muhimu, lakini kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog atalazimika kumuondoa mchezaji huyo katika programu yake ya kesho.
    Tayari Azam FC inawakosa Samih Haji Nuhu, Joseph Kimwaga, Ismail Gambo ‘Kussi Jr’, Farid Mussa na Ibrahim Mwaipopo ambao wote ni majeruhi kwa muda mrefu sasa.
    Ngongoro Heroes ilirejea nchini jana mchana kutoka Kenya ilikocheza na wenyeji na kutoa sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya Fainali za vijana Afrika na itaingia kambini keshokutwa kujiandaa na mchezo wa marudiano.
    Iwapo Ngorongoro Heroes itaitoa Kenya, raundi inayofuata itacheza na Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitafanyika mwakani nchini Senegal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIGO LINGINE AZAM FC IKIENDA KUIVAA RUVU SHOOTING UWANJA WA MABATINI KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top