Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
YANGA SC imefanya mazoezi Uwanja wa Kawe mjini Dar es Salaam na pamoja na habari njema za kurejea kwa kipa Deogratius Munishi ‘Dida’, lakini wachezaji wengine watano nyota hawakuwepo.
Mabeki wa kati wote, Kevin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hawakuwepo pamoja na viungo Athumani Iddi ‘Chuji’ na Haruna Niyonzima na mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Habari zinasema Cannavaro na Niyonzima wanaumwa, lakini hakukuwa na taarifa kuhusu kutokuwepo kwa Chuji, Yondan na Okwi.
Yanga SC ilirejea jana kutoka Tanga ambako ilifungwa mabao 2-1 na Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili.
Baada ya kupoteza pointi tatu zinazowafanya waachwe mbali na kidogo na Azam FC katika mbio za ubingwa, Yanga SC itashuka dimbani Jumapili hii kumenyana na timu nyingine ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na mbaya zaidi iko hatarini kuwakosa wachezaji wake hao ambao hawakuwepo mazoezini leo, iwapo matatizo yaliyowakwamisha yataendelea.
Azam FC inaongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23 ni ya tatu.
Wakati Yanga SC itacheza na JKT Ruvu Jumapili Uwanja wa Taifa, Mbeya City itacheza na Ashanti United Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Azam FC ilikuwa icheze Ruvu Shooting Jumapili hii pia, Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani lakini mchezo huo umesogezwa mbele hadi Aprili 9, kutokana na timu hiyo kuwa na wachezaji wengi katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Ngorongoro Heroes inatarajiwa kuondoka keshokutwa nchini kwenda Nairobi, Kenya kwa ajili ya mechi ya kuwania kucheza Fainali za Vijana Afrika, itakayochezwa Jumapili ya Aprili 6 mwaka huu Uwanja wa Machakos ulioko kilometa 80 kutoka jijini Nairobi na Azam ina wachezaji zaidi ya watano kwenye kikosi hicho.
Hao ni Aishi Manula, Bryson Raphael, Gardiel Michael, Kevin Friday, Mudathir Yahya, Farid Mussa na Hamad Juma.

Mwenzako anaumwa, wewe je? Haruna Niyonzima wa kwanza kushoto anaumwa, lakini Emmanuel Okwi anayemfuatia hakuwepo leo mazoezini Kawe bila sababu |

0 comments:
Post a Comment