// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OKWI, NIYONZIMA, YONDAN, CHUJI BADO HAWAJAINGIA KAMBINI YANGA SC, HUENDA WASIWEPO HATA KESHO DHIDI YA KAGERA SUGAR TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OKWI, NIYONZIMA, YONDAN, CHUJI BADO HAWAJAINGIA KAMBINI YANGA SC, HUENDA WASIWEPO HATA KESHO DHIDI YA KAGERA SUGAR TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 08, 2014

    OKWI, NIYONZIMA, YONDAN, CHUJI BADO HAWAJAINGIA KAMBINI YANGA SC, HUENDA WASIWEPO HATA KESHO DHIDI YA KAGERA SUGAR TAIFA

    Na Prince Akbar, Dar es Salaam
    YANGA SC itaendelea kuwakosa wachezaji wake Emmanuel Okwi, Kevin Yondan, Haruna Niyonzima, Athumani Iddi ‘Chuji’ na David Luhende katika mchezo wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kesho dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Yanga ilirudi kambini hoteli ya Kiromo, Bagamoyo baada ya mchezo wake juzi ikishinda 5-1 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa bila ya wachezaji hao ambao awali ilisema wataungana na wenzao baada ya mechi hiyo.
    Hawajapona? Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi bado hawajaingia kambini Yanga SC ikimenyana na Kagera Sugar kesho

    Yanga SC ilidai Yondan hakuungana na wenzake kambini kwa maandalizi ya mechi na JKT Ruvu baada ya kuomba kupumzika ili kutatua matatizo ya kifamilia- na benchi la Ufundi likampa ruhusa hiyo, kwa kuzingatia hawezi kucheza Jumapili kwa sababu alikuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
    Kuhusu David Luhende na viungo Haruna Niyonzima Athumani Idd ‘Chuji’ ilielezwa ni wagonjwa wakiwa wanaendelea na matibabu nao pia wataungana na wenzao baada ya mchezo wa Jumapili.
    Kuhusu Okwi walisema anaendelea na matibabu kufuatia kutonesha goti katika mchezo dhidi ya Mgambo JKT wakifungwa 2-1 wiki iliyopita Tanga, baada ya awali Okwi kuumia katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje kwa machela.
    Lakini hadi unaposoma habari hivi sasa, hakuna hata mmoja kati yao aliye kambini Kiromo, zaidi ya wachezaji wale wale walioshiriki mechi na JKT Ruvu Jumapili. 
    Hao ni makipa Juma Kaseja, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez, mabeki Juma Abdul, Mbuyu Twite, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Oscar Joshua na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakati viungo ni Frank Domayo, Said Dilunga, Nizar Khalfan, Salum Telela na Hamisi Thabit na washambuliaji Hussein Javu, Hamisi Kiza, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Jerry Tegete na Didier Kavumbagu.
    Yanga SC itashuka dimbani kesho kumenyana na Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu ikihitaji ushindi ili kujiweka sawa katika mbio za ubingwa dhidi ya Azam FC.
    Mabingwa hao watetezi wanazidiwa pointi nne na Azam FC iliyo kileleni kwa pointi zake 53 baada ya timu zote kucheza mechi 23, zikiwa zimebakiza mechi tatu kumalizia ligi. Azam FC yenyewe itamenyana na Ruvu Shooting Mlandizi kesho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI, NIYONZIMA, YONDAN, CHUJI BADO HAWAJAINGIA KAMBINI YANGA SC, HUENDA WASIWEPO HATA KESHO DHIDI YA KAGERA SUGAR TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top