// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); OKWI NI MGONJWA- YANGA SC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE OKWI NI MGONJWA- YANGA SC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, April 04, 2014

    OKWI NI MGONJWA- YANGA SC

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    YANGA SC imesema mshambuliaji wake Mganda, Emmanuel Okwi hayupo kambini kwa sababu ni mgonjwa na imewatetea pia na wachezaji wengine wawili ambao hawapo kambini eti nao ni wagonjwa.
    Taarifa ya Yanga SC katika tovuti yao imesema kwamba Kevin Yondan hakuungana na wenzake kambini baada ya kuomba kupumzika ili kutatua matatizo ya kifamilia- na benchi la Ufundi likampa ruhusa hiyo, kwa kuzingatia hawezi kucheza Jumapili dhidi ya JKT Ruvu Jumapili kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano na ataungana na wenzake baada ya Jumapili.
    Ugua pole jembe; Yanga SC imedai mshambuliaji wake Mganda Emmanuel Okwi ni mgonjwa ndiyo maana hayupo kambini

    Beki David Luhende na viungo Haruna Niyonzima Athumani Idd ‘Chuji’ ni wagonjwa wakiwa wanaendelea na matibabu nao pia wataungana na wenzao baada ya Jumapili.
    Taarifa hiyo imesema kwamba Okwi anendelea na matibabu kufuatia kutonesha goti katika mchezo dhidi ya Mgambo JKT mwishoni mwa wiki, baada ya awali Okwi kuumia katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje kwa machela.
    Taarifa imesema kocha Mkuu wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm kwa sasa ana wachezaji 20 kambini Kiromo Hotel, Bagamoyo, Pwani ambao ni makipa Juma Kaseja, Deo Munishi ‘Dida’ na Ally Mustafa ‘Barthez, mabeki Juma Abdul, Mbuyu Twite, Ibrahim Job, Rajab Zahir, Oscar Joshua na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakati viungo ni Frank Domayo, Said Dilunga, Nizar Khalfan, Salum Telela na Hamisi Thabit na washambuliaji Hussein Javu, Hamisi Kiza, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Jerry Tegete na Didier Kavumbagu.
    Aidha, Yanga SC imekiri kuwasilisha barua ya malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya mchezaji Mohamed Hussein Neto kuchezea Mgambo JKT bila kuwa na Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) wala kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini. Yanga SC imedai mchezaji huyo ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na jina lake halisi ni Noel Melondoo.
    Hamkani si shwari Yanga SC baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mgambo JKT Jumapili hivyo kuchwa mbali kidogo na Azam FC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Wiki hii magazeti nchini yameandika kwamba Okwi amesusa kwa kuwa anadai sehemu ya fedha zake za usajili na Yondan amesusa baada ya kusemewa ovyo kwa kusababisha penalti iliyoipa bao la ushindi Mgambo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI NI MGONJWA- YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top