MKANGANYIKO umeibuka, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kugomea kipengele cha 26 katika rasimu ya Katiba mpya ya klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam.
Ni TFF iliyotoa maelekezo kwa wanachama wake kufanyia marekebisho ya Katiba zake, na ikatoa angalizo zizingatie Katiba yao (TFF) na FIFA.
Inafahamika, FIFA pamoja na kutoa mwongozo wa aina za Katiba za wanachama wake, lakini pia imeagiza Katiba hizo zisipingane na Katiba za nchi zao.
TFF imesema kwa kuwa pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu sifa za mgombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF, hivyo basi Kamati imeagiza kipengele hicho kibaki vilevile bila kubadilishwa.
Nasema mkanganyiko, kwa sababu awali ilielezwa TFF waliandika barua kwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi juu ya kipengele hicho, lakini kabla majibu hayajajulikana, tayari imeatoa uamuzi.
Simba SC wanahangaikia mustakabli wa klabu yao baada ya kupitia wakati mgumu kwa mwaka wa pili sasa na wanataka Katiba yao mpya itoe wigo mpana wa watu kujitokeza kugombea, ili wachuje pumba na mchele.
Lakini sasa TFF inaelekea kuwabana wasiweze kutimiza dhamira yao hiyo- si vibaya kama watakuwa na hoja za msingi na za wazi katika hilo, ili wana Simba SC wajiridhishe.
Lakini kwa maelezo mafupi tu ya kukataa kipengele hicho bila sababu za kuridhisha, wakati inafahamika nchi nyingine wanachama wa FIFA, likiwemo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) vimechana na kipengele ambacho TFF bado wanaamini.
Ni mkanganyiko, kwa sababu wakati TFF ikigombea kipengele hicho, inasema vipengele vingine vyote vimepitishwa na vitapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya kusajiliwa.
Aidha, TFF imesema mchakato wa uchaguzi wa Simba uendelee kama ulivyopangwa wakizingatia uamuzi huo wa Kamati.
Lakini wakati huo huo, TFF imesema kwamba Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imeshauri TFF kuwasiliana na FIFA kupata mwongozo kuhusu katazo la watu wenye rekodi ya kifungo kugombea na imeahidi kuufanyia kazi na kama kuna mabadiliko yoyote kiutaratibu yataanzia katika Katiba ya TFF kupitia Mkutano Mkuu.
Mkanganyiko, tayari TFF imeruhusu mchakato wa uchaguzi wa Simba SC uendelee na wakati huo inasema itayafanyia kazi mapendekezo ya Kamati ya Sheria na kama kuna mabadiliko yoyote kiutaratibu yataanzia katika Katiba ya TFF kupitia Mkutano Mkuu.
Hapa maana yake Simba SC watalazimika kufanya aina ya uchaguzi ambao hautokani na matakwa yao- iwapo watafuata mwongozo huo wa TFF.
Vigumu kujua nini kipo nyuma ya haya yote na ni kwa maslahi ya nani, lakini uamuzi huu wa TFF unaleta mkanganyiko mkubwa na kuwarudisha nyuma Simba SC.
Suala jepesi la kujiuliza baada ya maelezo yote, je ni sahihi Katiba ya TFF kupingana na Katiba halali ya nchi yetu ya sasa? Alamsiki.

0 comments:
Post a Comment