// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NANI KAMA MRISHO NGASSA YANGA AFRICA? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NANI KAMA MRISHO NGASSA YANGA AFRICA? - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, April 06, 2014

    NANI KAMA MRISHO NGASSA YANGA AFRICA?

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    MRISHO Khalfan Ngassa leo amefunga hat trick yake ya kwanza katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu Yanga SC ikiichapa 5-1 JKT Ruvu na kutimiza mabao 12 katika kinyanga’nyiro cha ufungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hat trick hiyo inafanya jumla ya mabao aliyofunga Ngassa tangu arejee Yanga SC msimu huu katika mashindano yote kufika 20 katika mechi 28. 
    Mrisho Ngassa amefikisha mabao 20 Yanga SC ndani ya mechi 28

    Ngassa sasa anashika nafasi ya tatu kwa ufungaji wa mabao mengi kwenye Ligi Kuu msimu huu, nyuma ya Amisi Tambwe wa Simba SC mabao 19 na Kipre Tchetche wa Azam FC 13. 
    Msimu uliopita Mrisho Ngassa akiwa Simba SC alifunga mabao saba tu katika mechi 27, wakati sasa Ligi Kuu ikiwa inaelekea ukingoni, mchezaji huyo amekwishafunga mabao 20 katika mechi 26.
    Mabao 12 amefunga katika Ligi Kuu, wakati mengine amefunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika na mechi za kirafiki.
    Ikumbukwe Ngassa aliuanzia nje msimu huu, akikosa mechi sita baada ya kufungiwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kubaini alisaini Yanga SC akiwa ana mkataba na Simba SC pia.
    Ngassa alitua Simba SC msimu uliopita akitokea Azam FC ambao walimtoa kwa mkopo baada ya kukerwa na tabia zake na Kamati pia ilimuauru kurudisha Sh. Milioni 30 alizochukua kusaini Mkataba na Wekundu wa Msimbazi pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15).
    Ngassa hakucheza mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam na akakosa mechi tano za mwanzo za Ligi Kuu, lakini pamoja na hayo ana mabao 12 kwenye ligi hiyo pekee, mbele ya Hamisi Kiiza aliyefunga mabao 11.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NANI KAMA MRISHO NGASSA YANGA AFRICA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top