KOCHA wa Manchester United, David Moyes amemuambia refa wa Hispania, Carlos Carballo kutoa maamuzi sahihi katika mchezo wao dhidi ya mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich kutokana na tabia ya wachezaji wa timu hiyo kujirusha kujiangusha.
United inatakutana na mabingwa wa Bundesliga leo Uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa kwanza wa kwanza wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya. Bayern inapewa nafasi kubwa ya kushinda, lakini timu hiyo ya kocha Pep Guardiola ilishutumiwa baada ya kuitoa Arsenal katika raundi iliyopita, kwa Arsene Wenger kumlaumu Arjen Robben kuwa hodari wa kujirusha kujiangusha.
Moyes alisema: "Tunawaamini marefa watafanya uamuzi sahihi. Kujirusha ni moja ya vitu vibaya vya kufanyia kazi. Ningependa kutahadharisha juu ya hilo, lakini nisingependa kumlenga mchezaji binafsi,".
Winga Mholanzi Anayepaa: Nyota wa Bayern, Arjen Robben amekuwa akishutumiwa kwa kujiangusha kirahisi
Angalizo la tahadhari: Kocha wa Manchester United, David Moyes anatumai refa Carlos Velasco Carballo atwaadhibu wachezaji wa kujiangusha
Wajerumani hao tayari wamekwishatetea ubingwa wa Bundesliga na wameshinda mechi zao 27 kati ya 30 zilizopita kwenye mashindano yote. Lakini Ryan Giggs bado anaamini United inaweza kufika fainali.
Muongo mkubwa: Arsene Wenger alimshutumu Robben kwa tukio hili alipojiangusha wakati alipokutana na kipa Wojciech Szczesny katika raundi iliyopita
0 comments:
Post a Comment