// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MFILIPINO WA KUZIPIGA NA MIYEYUSHO AWASILI KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MFILIPINO WA KUZIPIGA NA MIYEYUSHO AWASILI KESHO DAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 02, 2014

    MFILIPINO WA KUZIPIGA NA MIYEYUSHO AWASILI KESHO DAR

    Na Asha Said, Dar es Salaam
    BONDIA Ronald Pontillas, atawasili nchini kesho asubuhi  kwa ajili ya pambano lake la kimataifa dhidi ya bondia  Francis Miyeyusho, litakalofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
    Akizungumza Dar es Salaam jana, mratibu wa pambano hilo Mussa Kova, alisema kuwa Pontillas raia wa Ufilipino,  atawasili nchini akiwa na kocha wake Amogo Samson.
    Kova alisema bondia huyo atawasili majira ya saa moja asubuhi, akitumia ndege ya Qatar Airways.
    Ronald Pentilla atawasili kesho Dar es Salaam

    Alisema kuwa moja kwa moja ataenda hotelini kupomzika kabla ya saa 5, kuzungumza na vyombo vya habari.
    Kova alisema kuwa maandalizi mengine yanaendelea vizuri ambapo, hata suala la viingilio nalo tayari limeshapangwa.
    Alisema katika viingilio vitakuwa vya aina mbili ambavyo ni Sh.20,000 kwa VIP na kawaida itakuwa sh.10,000.
    Alisema kuwa katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambayo atayatangaza kesho katika mkutano maalum na vyombo vya habari.
    Pia  Kova alisema maandalizi yanakwenda vizuri na 
    kusisitiza kuwa litasimamiwa na chama cha 
    ngumi za kulipwa Tanzania (PST).
    "Mabondia wote wako katika hali nzuri ya ushindani, tunategemea Miyeyusho atafanya vizuri na kukabiliana na upinzani wa mpinzani wake kwani ni bondia mzuri na mwenye kiwango cha
    juu," alisema Kova.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MFILIPINO WA KUZIPIGA NA MIYEYUSHO AWASILI KESHO DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top