Na Princess Asia, Nairobi
SAFARI ya kwenda Fainali za 19 za michuano ya vijana Afrika chini ya umri wa miaka 20 nchini Senegal mwaka 2015 inaanza wikiendi hii kwa mechi za kwanza kuchezwa viwanja mbalimbali nchi tofauti.
Zaidi ya timu 20 zitashiriki hatua ya kwanza kuwania nafasi saba za kushiriki Fainali za michuano hiyo barani.
Timu za Kusini mwa Afrika tupu, Msumbiji na Namibia zitamenyana mjin Maputo wakati Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, wenyeji Malawi wataikaribisha Botswana.
Swaziland itaikaribisha Lesotho, Burundi itasafiri hadi Djibouti wakati Shelisheli watakuwa wenyeji wa Ethiopia na kocha mpya wa Gambia, Mustapha Manneh aliyeteuliwa mwezi uliopita atakuwa na mtihani dhidi ya Liberia mjini Monrovia.
Sierra Leone itamenyana na Guinea mjini Freetown wakati Niger na Kongo zitapambana mjini Niamey, huku nyasi za Uwanja wa El-Menzah mjini Tunis zikiwaka moto kwa mchezo kati Tunisia na Mauritania wakati Kenya watakuwa wenyeji wa Tanzania mjini Kisumu.
Mechi za marudiano zitachezwa wikiendi ya kati ya Aprili 25 na 27 na washindi wataungana na mabingwa watetezi Misri, Angola, Benin, Burkina Faso, Cameroon, DRC, Gabon, Ghana, Mali, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia katika Raundi ya Pili.
Fainali za michuano hiyo zitafanyika kuanzia Machi 8 hadi 22 mwakani nchini Senegal na timu zitakazotinga Nusu Fainali zitashiriki Kombe la Dunia la FIFA la U-20 nchini New Zealand.

Timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 mwaka juzi |

0 comments:
Post a Comment