// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); MBEYA CITY YAFIKISHA POINTI ZA YANGA 46 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE MBEYA CITY YAFIKISHA POINTI ZA YANGA 46 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, April 05, 2014

    MBEYA CITY YAFIKISHA POINTI ZA YANGA 46

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    MBEYA City imelazimishwa sare ya bila kufungana na Ashanti United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam hivyo kushindwa kuiengua Yanga SC nafasi ya pili pamoja na kuifikia kwa pointi.
    Sare hiyo inaifanya Mbeya City ifikishe pointi 46 sawa na Yanga SC, ambayo inaendelea kukaa nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao. Hata hivyo, Mbeya City imecheza mechi mbili zaidi ya Yanga. 
    Ashanti ilimaliza mechi hiyo ikiwa pungufu, baada ya mchezaji wake Ally Abdallah kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 89 kwa kumchezea rafu Deogratius Julius.
    Beki wa Ashanti United, Iddi Silas aliyeruka juu kupambana na mshambuliaji wa Mbeya City, Mwagane Yeya 

    Ashanti inayofundishwa na kocha mkongwe Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ilicheza soka maridadi na kutawala sehemu ya kiungo muda wote wa mchezo, lakini wakashindwa kutumia vizuri nafasi walizotengeneza.
    Deus Kaseke wa Mbeya City akimtoka Abuu Mtiro wa Ashanti United
    Mbeya City leo ilitumia mipira mirefu kushambulia na dakika ya tano Paul Nonga alikosa bao la wazi akiwa mita tatu kutoka langoni alipounganishia nje pasi nzuri ya Steven Mazanda.
    Beki wa Ashanti, Shaffih Hassan akiruka kupiga kichwa dhidi ya Deus Kaseke wa Mbeya City na kushoto Hassan Kabunda akiwa tayari kutoa msaada
    Hassan Mwasapili wa Mbeya City akimtoka Joseph Mahundi wa Ashanti kushoto 

    Saad Kipanga aliwasumbua mno mabeki wa Ashanti, lakini akashindwa kufunga tu, wakati Mwagane Yeya aliyeingia dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Alex Sethi alidhibitiwa.
    Kikosi cha Mbeya City; David Burhan, Aziz Sibo, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Yohana Morris, Anthony Matogolo, Alex Sethi/Mwagane Yeya dk67, Steven Mazanda/Kemy Ally dk65, Paul Nonga, Saad Kipanga na Deus Kaseke. 
    Ashanti United; Soud Abdallah, Anthony Matangalu/Hussein Mkongo dk55, Abuu Mtiro, Shaffih Hassan, Mohammed Fakhi, Iddi Silas, Hassan Kabunda, Mussa Nampaka, Paul Maona/Ike Obinna dk43, Ali Mohammed na Joseph Mahundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MBEYA CITY YAFIKISHA POINTI ZA YANGA 46 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top