Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
MBEYA City itapanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara iwapo itaifunga Ashanti United kesho Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Ligi hiyo kesho inaingia raundi ya 24, Azam FC inaongoza kwa pointi zake 53 baada ya kucheza mechi 23, ikifuatiwa na Yanga SC yenye pointi 46 za mechi 22 na Mbeya City yenye pointi 45 za mechi 23 ni ya tatu.
Kagera Sugar itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kesho.
Ashanti United inayofundishwa na Abdallah Kibaden ipo katika mkakati wa kukwepa kushuka daraja.
Keshokutwa (Aprili 6 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Coastal na Mgambo Shooting Stars (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT na Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers na Mtibwa Sugar (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Yanga dhidi ya JKT Ruvu (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam).
Raundi hiyo itakamilika Aprili 9 mwaka huu kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Kikosi cha Mbeya City |

0 comments:
Post a Comment