Na Prince Akbar, Dar es Salaam
WAWAKILISHI wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), TP Mazembe na AS Vita wamepangwa kundi moja, A katika Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyo kwa Esperance na C.S Sfaxien za Tunisia ambazo zipo kundi B pamoja na E.S Setif ya Algeria na Ahly Benghazi ya Libya.
Mabingwa mara tano wa michuano hiyo, Zamalek ya Misri wapo pia Kundi A na wababe hao wa DRC na vigogo wa Sudan, Al Hilal.
Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22 na 24 huku timu zitakazoshika nafasi mbili za juu kwenye makundi zikisonga Nusu Fainali.
MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Kundi A: TP Mazembe (DRC), Al-Hilal (Sudan), Zamalek (Misri) na AS Vita (DRC)
Kundi B: Esperance (Tunisia), CS Sfaxien (Tunisia),
Entente Setif (Algeria) na Al-Ahly Benghazi (Libya).

Vijana wa kazi; Washambuliaji tegemeo wa TP Mazembe, Watanzania Mbwana Samatta kulia na Thomas Ulimwengu kushoto wamepangwa kundi moja na AS Vita ya DRC pia |
Mechi zinatarajiwa kuchezwa kuanzia kati ya Mei 16 na 18 na 23 na 25, Juni 6 na 8, Julai 25 na 27, Agosti 8 na 10 na 22 na 24 huku timu zitakazoshika nafasi mbili za juu kwenye makundi zikisonga Nusu Fainali.
MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
Kundi A: TP Mazembe (DRC), Al-Hilal (Sudan), Zamalek (Misri) na AS Vita (DRC)
Kundi B: Esperance (Tunisia), CS Sfaxien (Tunisia),
Entente Setif (Algeria) na Al-Ahly Benghazi (Libya).
0 comments:
Post a Comment