Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Yanga SC, Alhaj Yussuf Mehboob Manji amekwishasema hatatetea nafasi yake hiyo katika uchaguzi ujao- ambao leo imetangazwa utafanyika Juni 15, mwaka huu.
Taarifa ya tovuti ya klabu hiyo bingwa ya zamani nchini, imesema kikao cha Kamati ya Utendaji kilichoketi Aprili 10, mwaka huu makao makuu ya klabu, kiliazimia Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Yanga SC ufanyike Juni 15, mwaka huu.
Hata hivyo, kuhusu taratibu nzima za mchakato wa uchaguzi, imeelezwa zitatangazwa baadaye na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Wakili Alex Mgongolwa.
Manji aliingia madarakani Julai 14, mwaka juzi katika uchaguzi mdogo wa klabu hiyo uliofanyika kufuatia baadhi ya viongozi kujiuzulu, akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti Wakili Lloyd Nchunga na makamu wake, Davis Mosha na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kama Mze Yussuf.
Miongoni mwa walioziba nafasi hizo pamoja na Manji ni Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe Abdallah Mbaraka au Abdallah Bin Kleb na Mussa Katabaro.
Baada ya Yanga kufungwa mabao 3-1 na matani wake Simba SC Desemba 21, mwaka jana katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Manji aliwaambia wanachama wa klabu hiyo yeye hatagombea tena.

Siku za kuondoka zimekaribia; Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji kulia akiwa na Makamu wake Clement Sanga kushoto. |
Hata hivyo, kuhusu taratibu nzima za mchakato wa uchaguzi, imeelezwa zitatangazwa baadaye na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, Wakili Alex Mgongolwa.
Manji aliingia madarakani Julai 14, mwaka juzi katika uchaguzi mdogo wa klabu hiyo uliofanyika kufuatia baadhi ya viongozi kujiuzulu, akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti Wakili Lloyd Nchunga na makamu wake, Davis Mosha na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kama Mze Yussuf.
Miongoni mwa walioziba nafasi hizo pamoja na Manji ni Makamu wake, Clement Sanga na Wajumbe Abdallah Mbaraka au Abdallah Bin Kleb na Mussa Katabaro.
Baada ya Yanga kufungwa mabao 3-1 na matani wake Simba SC Desemba 21, mwaka jana katika mechi ya Nani Mtani Jembe, Manji aliwaambia wanachama wa klabu hiyo yeye hatagombea tena.
0 comments:
Post a Comment