WACHEZAJI wa Manchester United wamezuru makaburi ya wachezaji wa timu hiyo waliofariki katika ajali ya ndege mwaka 1958 mjini Munich kuelekea mchezo wa marudiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Kiungo wa United, Michael Carrick alisema alivutiwa na kikundi cha mashabiki wa Mashetani hao Wekundu kilichosafiri kwenda kuisapoti timu walivyokuwa wanaimba wakati walipozuru eneo la hilo la kihistoria nchini Ujerumani.
"Kutoa heshima zetu katika kumbukumbu ya Munich, na nilivyovutiwa na wimbo wa mashabiki "Man utd haitakufa",' Carrick aliposti kwenye Twitter.
Heshima: Wachezaji wa Manchester United na kocha David Moyes wamezuru makaburi ya wachezaji wa timu hiyo waliofariki kwa ajali ya ndege mjini Munich
Heshima: Kocha wa United, Moyes akiweka shada la maua
Nyota wa United wakitoa heshima zao katika jiwe la kumbukumbu mjini Munich
Heshima: Mashabiki wa Manchester United wakitoa heshima zao Jumanne
United pia walizuru Uwanja wa Allianz Arena ambako watamenyana na Bayern Jumatano wakitakiwa kushinda baada ya mchezo wa kwanza kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Old Trafford na mabingwa hao wa Ulaya.
Wayne Rooney akitabasamu wakati United ilipozuru Allianz Arena
Moyes na mkongwe Darren Fletcher wakizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari kuelekea mchezo na Bayern Munich
0 comments:
Post a Comment