KLABU ya Manchester City ipo karibu kumsajili beki mwenye thamani ya Pauni Milioni 20, Eliaquim Mangala wa FC Porto.
Vyanzo nchini Ureno vinasema kwamba Mkurugenzi wa Michezo, Txiki Begiristain alikwenda mjini Porto maalumu kumuangali beki huyo ghali akicheza dhidi ya Sevilla katika Europa League.
Mangala alifunga bao nla ushindi timu hiyo ya Luis Castro na Begiristain inatumai kukamilisha dili hilo la beki huyo mwenye umri wa miaka 23 kuelekea msimu ujao ahamie Manchester.
Anatakiwa: Beki ghali alitazamwa na Mkurugenzi wa City, Txiki Begiristain akicheza Europa League
Mchezaji huyo wa zamani wa Standard Liege alikaribia kujiunga na timu hiyo ya Uwanja wa Etihad Januari, mwaka huu lakini dau la City la Pauni Milioni 38 kwa ajili ya kuchukua wachezaji wawili, Mfaransa huyo na mchezaji mwenzake, Fernando lilikufa katika siku ya mwisho ya uhamisho.
Pamoja na hayo, City iliendelea na dhamira ya kutaka kumsajili mchezaji huyo na ikiwa kila kitu kitakwenda kulingana na mipango ya City, Mangala atatua Etihad kabla ya mwanzo wa msimu ujao.
Habari hizo zitapokewa kama pigo kwa Chelsea, ambayo pia ilionyesha nia ya kumsajili Mangala miezi ya karibuni.
Mangala ameichezea mechi mbili timu ya taifa ya Ufaransa, ingawa hawezi kucheza Ubelgiji ambako alihamia katika mji wa Namur kutoka Parisian, kitongoji cha Colombes akiwa na umri wa miaka mitano.
WASIFU WA ELIAQUIM MANGALA...
Februari 13, 1991 - Alizaliwa mjini Colombes, Ufaransa. Akahamia Namur, Ubelgiji akiwa na umri wa miaka mitano
2004 - Akasajiliwa na timu ya daraja la nne Ubelgiji, Union Royale Namur
2008 - Akachukuliwa na Standard Liege ya Ubelgiji
Novemba 2008 - Akacheza mechi ya kwanza kama mchezaji wa kulipwa akiingia dakika ya 89 kutokea benchi
2008/2009 - Alishinda taji la Ligi Kuu ya Ubelgiji akiwa na Standard, ingawa alicheza mechi 11 tu
Septemba 2009 - Alifunga katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya
Novemba 2009 - Aliteuliwa kuichezea timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 ya Ufaransa kutoka Ubelgij
2010/2011 - Alikuwa mchango mkubwa kwa kikosi kilichotwaa Kombe la Ubelgiji
Agosti 2011 - Alijiunga na vigogo wa Ureno, FC Porto kwa ada ya uhamisho ya Euro Milioni 6.5
2011/2012 - Alishinda Primeira Liga akiwa na Porto
2012/2013 - Aliisaidia Porto kutetea vizuri taji hilo
Juni 2013 - Aliichezea mechi ya kwanza Ufaransa ikifungwa 1-0 na Uruguay
0 comments:
Post a Comment