Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
TIMU ya vijana ya Kenya inatarajiwa kuwasili nchini leo (Aprili 25 mwaka huu) saa 1 usiku tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania (Ngorongoro Heroes).
Mechi hiyo ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 itachezwa Jumapili (Aprili 27 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 na sh. 5,000.
Kenya na Ngorongoro Heroes zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machakos wiki tatu zilizopita. Mshindi baada ya mechi ya marudiano atacheza na Nigeria katika raundi itakayofuata.
Ngorongoro Heroes inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo chini ya Kocha John Simkoko. Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana wakati Kamishna ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.

Kipa wa Ngorongoro, Aishi Manula anatarajiwa kuibeba timu hiyo Jumapili |
Kenya na Ngorongoro Heroes zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyochezwa Machakos wiki tatu zilizopita. Mshindi baada ya mechi ya marudiano atacheza na Nigeria katika raundi itakayofuata.
Ngorongoro Heroes inaendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo chini ya Kocha John Simkoko. Mechi hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi wakiongozwa na Pacifique Ndabihawenimana wakati Kamishna ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.
0 comments:
Post a Comment