Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
WINGA Simon Msuva na mshambuliaji Didier Kavumbangu leo watacheza mechi ya 60 kila mmoja tangu wajiunge na Yanga SC mwaka juzi, iwapo watapangwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar.
Yanga SC itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar ya Bukoba leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo ambao wanahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kutetea ubingwa.
Msuva na Kavumbangu walipishana miezi miwili tu kuingia Yanga SC, lakini hadi sasa wote wamekwishacheza mechi 59.
Msuva alianza kuichezea Yanga SC katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwaka juzi akiiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa ikiwa chini ya kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet.
Kavumbangu alimvutia Saintfiet kwenye michuano hiyo ya Kagame akiwa anaichezea klabu ya Atletico ya kwao Burundi na akamsajili baada ya mashindano hayo.
Pamoja na kwamba Mbelgiji huyo alifukuzwa baada ya mechi tatu za msimu huo wa Ligi Kuu na nafasi yake kuchukuliwa na Mholanzi, Ernie Brandts ambaye naye alifukuzwa Desemba mwaka jana na kuajiriwa Mholanzi mwingine, Hans van der Pluijm, lakini Kavumbangu ameendelea kufanya vizuri Jangwani.
Katika mechi 59 alizocheza hadi sasa, tayari Kavumbangu amefunga mabao 29 kwenye mashindano yote likiwemo moja la penalti wakati Msuva amefunga mabao 12.
Mabingwa hao watetezi wanazidiwa pointi nne na Azam FC iliyo kileleni kwa pointi zake 53 baada ya timu zote kucheza mechi 23, zikiwa zimebakiza mechi tatu kumalizia ligi. Azam FC yenyewe itamenyana na Ruvu Shooting Mlandizi leo.

Mechi ya 60; Simon Msuva tayari ameichezea Yanga SC mechi 59 zikiwemo zisizo za mashindano |
Msuva alianza kuichezea Yanga SC katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mwaka juzi akiiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa ikiwa chini ya kocha Mbelgiji, Tom Saintfiet.
Kavumbangu alimvutia Saintfiet kwenye michuano hiyo ya Kagame akiwa anaichezea klabu ya Atletico ya kwao Burundi na akamsajili baada ya mashindano hayo.
Pamoja na kwamba Mbelgiji huyo alifukuzwa baada ya mechi tatu za msimu huo wa Ligi Kuu na nafasi yake kuchukuliwa na Mholanzi, Ernie Brandts ambaye naye alifukuzwa Desemba mwaka jana na kuajiriwa Mholanzi mwingine, Hans van der Pluijm, lakini Kavumbangu ameendelea kufanya vizuri Jangwani.
Didier Kavumbangu amekuwa mchezaji muhimu kwa kipindi chote cha kuwapo kwake Yanga SC |
Katika mechi 59 alizocheza hadi sasa, tayari Kavumbangu amefunga mabao 29 kwenye mashindano yote likiwemo moja la penalti wakati Msuva amefunga mabao 12.
Mabingwa hao watetezi wanazidiwa pointi nne na Azam FC iliyo kileleni kwa pointi zake 53 baada ya timu zote kucheza mechi 23, zikiwa zimebakiza mechi tatu kumalizia ligi. Azam FC yenyewe itamenyana na Ruvu Shooting Mlandizi leo.
0 comments:
Post a Comment