Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
SHOMARY Kapombe amejiunga na klabu ya Azam FC kufanya mazoezi ili kujiweka fiti kwa wakati huu ambao hana timu baada ya kugoma kurejea klabu yake ya Daraja la Nne Ufaransa, AS Cannes.
Tovuti ya Azam FC imemnkukuu Kapombe akisema kwamba ameamua kuja kufanya Azam FC kwa sababu kwanza ni jirani na eneo analoishi na pia wana vifaa vyote vya vya mazoezi vitakavyosaidia kumuweka fiti.
Hata hivyo, Kapombe hakutaka kuzama ndani juu ya mustakabali wake wa baadaye, akisema; “Nimekuja Azam kufanya mazoezi kujiweka fiti tu, basi,”alisema.
Tayari kuna habari kwamba, Kapombe anataka kucheza klabu ya Tanzania ambayo itashiriki michuano ya Afrika mwakani.
Kiungo huyo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, anamaliza Mkataba wake Simba SC mwezi huu, lakini alikwishaingia Mkataba wa miaka minne na AS Cannes ya Ufaransa mwaka jana.
Na Simba SC imekubaliana na klabu ya Daraja la Nne Ufaransa, kuununua Mkataba wa mchezaji huyo arejee kufanya kazi Msimbazi baada ya kushindwa kuendelea kucheza Ulaya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alizungumza na AS Cannes mwezi uliopita na kufikia makubaliano ya kuuziana Mkataba huo, ili Kapombe arejee Msikmbazi.
Poppe alisema kwamba Simba SC imekubali kuilipa Cannes kiasi cha Euro 33, 000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.
Kapombe alitolewa bure kwenda AS Cannes katikati ya mwaka jana akiwa bado ana Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi, unaomalizika Aprili mwaka huu.
Baada ya kuwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi mitatu, Kapombe alirejea nchini Novemba mwaka jana kwa ruhusa maalum ya kuja kuichezea timu ya taifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.
Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo akaamua kubaki moja kwa moja nyumbani akidai halipwi mishahara.

Kijana Chamazi; Shomary Kapombe kulia akifurahia jambo na mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco jioni hii Uwanja wa Azam Complex |
Hata hivyo, Kapombe hakutaka kuzama ndani juu ya mustakabali wake wa baadaye, akisema; “Nimekuja Azam kufanya mazoezi kujiweka fiti tu, basi,”alisema.
Tayari kuna habari kwamba, Kapombe anataka kucheza klabu ya Tanzania ambayo itashiriki michuano ya Afrika mwakani.
Kiungo huyo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, anamaliza Mkataba wake Simba SC mwezi huu, lakini alikwishaingia Mkataba wa miaka minne na AS Cannes ya Ufaransa mwaka jana.
Na Simba SC imekubaliana na klabu ya Daraja la Nne Ufaransa, kuununua Mkataba wa mchezaji huyo arejee kufanya kazi Msimbazi baada ya kushindwa kuendelea kucheza Ulaya.
Shomary Kapombe akiwa mazoezini Chamazi |
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alizungumza na AS Cannes mwezi uliopita na kufikia makubaliano ya kuuziana Mkataba huo, ili Kapombe arejee Msikmbazi.
Poppe alisema kwamba Simba SC imekubali kuilipa Cannes kiasi cha Euro 33, 000 ambazo sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa mchezaji wake huyo.
Kapombe alitolewa bure kwenda AS Cannes katikati ya mwaka jana akiwa bado ana Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi, unaomalizika Aprili mwaka huu.
Baada ya kuwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi mitatu, Kapombe alirejea nchini Novemba mwaka jana kwa ruhusa maalum ya kuja kuichezea timu ya taifa katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe.
Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo akaamua kubaki moja kwa moja nyumbani akidai halipwi mishahara.
0 comments:
Post a Comment