// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KANUNI ZA LIGI KUU ZINAVYOSEMA KUHUSU RUFAA YA YANGA, POINTI ZA CHEE NI IWAPO... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KANUNI ZA LIGI KUU ZINAVYOSEMA KUHUSU RUFAA YA YANGA, POINTI ZA CHEE NI IWAPO... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, April 06, 2014

    KANUNI ZA LIGI KUU ZINAVYOSEMA KUHUSU RUFAA YA YANGA, POINTI ZA CHEE NI IWAPO...

    Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
    YANGA SC imewasilisha malalamiko Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa mshambuliaji wa Mgambo Shooting Stars, Mohammed Neto ambaye alicheza dhidi yao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Jumapili iliyopita si raia wa Tanzania na hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
    Ingawa malalamiko hayo yamewasilishwa nje ya muda (time barred), lakini TFF imeyapokea na imesema itayawasilisha kwenye Kamati husika kwa ajili ya kupitiwa na baadaye kutolewa uamuzi.
    Mohamed Neto au Noel Melondoo kwa mujibu wa Yanga SC

    Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko yote kuhusu mchezo yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya saa 24 baada ya mchezo kumalizika na Yanga waliwasilisha malalamiko hayo nje ya muda.
    Lakini nini mustakabali wa malalamiko hayo?
    Aya ya kwanza ya kanuni ya 61 ya Ligi Kuu ya Bara inayozungumzia adhabu zinazohusu usajili na uhamisho inasema; “Mchezaji yeyote atakayebadili jina lake halisi kwa madhumuni ya kudanganya ili asajiliwe kinyume cha masharti ya Kanuni hizi, atafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili kuanzia tarehe ya kubainika,”. Aya ya pili ya kanuni hiyo inasema; “Klabu iliyomchezesha mchezaji aliyebadili jina kwa nia ya kudanganya italipa faini ya TShs 1,000,000/= kwa kila mchezo ambao mchezaji huyo alicheza, lakini matokeo ya uwanjani hayatobadilika,”.
    Kwa kanuni hizi- maana yake Yanga SC haitanufaika na pointi za chee baada ya kufungwa 2-1 na Mgambo JKT katika mchezo huo wa Ligi Kuu iwapo itabainika Neto alidanganya jina ili kusajiliwa na Mgambo kwa kukwepa ugumu wa kupata ITC.
    Lakini kanuni hiyo hiyo aya ya tatu inasema; “Klabu itayothibitika kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa na klabu hiyo, itapoteza michezo husika, kitalipa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000/=) na mchezaji husika atafungiwa kwa kwa kipindi kisichopunguwa miezi kumi na miwili (12) bila ya kujali kukatwa au kutokatwa rufaa,”.
    Kwa mujibu wa malalamiko ya Yanga SC, Neto au Noel Melondoo habanwi na aya ya tatu ya kanuni ya 61, bali adhabu yake inaweza kupatikana kutoka aya ya kwanza na ya pili ya kanuni hiyo, iwapo itabainika ni kweli alifanya udanganyifu.
    Baada ya kufungwa na Mgambo JKT, Yanga SC imeachwa kwa pengo la pointi saba na Azam FC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu-53 kwa 46.
    Iwapo Yanga SC itapoteza mchezo wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam basi Azam itahitaji kushinda dhidi ya Ruvu Shooting Jumatano kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu, ikiwa ina mechi mbili mkononi- kwani itafikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KANUNI ZA LIGI KUU ZINAVYOSEMA KUHUSU RUFAA YA YANGA, POINTI ZA CHEE NI IWAPO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top