// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); KAMA SI UTAPELI HII TUITE NINI? MECHI YA RUVU NA AZAM WATU WALIPISHWA VIINGILIO MARA MBILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE KAMA SI UTAPELI HII TUITE NINI? MECHI YA RUVU NA AZAM WATU WALIPISHWA VIINGILIO MARA MBILI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, April 11, 2014

    KAMA SI UTAPELI HII TUITE NINI? MECHI YA RUVU NA AZAM WATU WALIPISHWA VIINGILIO MARA MBILI

    Na Baby Akwitende, Mlandizi
    MASHABIKI wa soka kutoka sehemu mbalimbali ambao walijitokeza kwenye Uwanja wa Mabatini mjini hapa kuhuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara wamelalamika kutapeliwa na Bodi ya Ligi kufuatia kulipishwa kiingilio mara mbili.
    Akizungumza baada ya mechi kati ya Ruvu Shooting na Azam kumalizika, mmoja wa mashabiki hao, Robert Munisi, alisema kuwa anashangaa kuona leo wamelipishwa tena wakati jana wakati alipolipa na mechi hiyo kuahirishwa waliambiwa watunze vishina vya tiketi zao.
    Robert Munisi akilalamika kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, Geoffrey Nyange 'Kaburu' juu ya watu kulipishwa viingilio mara mbili mechi ya Ruvu Shooting na Azam FC

    Munisi alisema kwamba tukio hilo limewahuzunisha na si ustaarabu kwa sababu limeonyesha kuwadharau mashabiki wa mchezo huo.
    Alisema kwamba hali hiyo inasababisha uaminifu na uadilifu kwenye mchezo wa soka kupungua.
    “Inasikitisha sana, jana tulielezwa kwamba tutunze vishina vya tiketi zetu lakini leo wamekataa kuvitambua na kutueleza tununue tiketi nyingine,’ alilalamika Munisi ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Arusha Mjini (ADFA).
    Shabiki mwingine, Afande Japhet, wa Kibaha Maili moja alisema kwamba endapo jana wangeona mechi au japo timu zikipasha wasingelalamika.
    Japhet alisema hali hiyo si njema kuendelea kufanyika na kama mashabiki wangekuwa wengi kwenye uwanja mkubwa hali ingekuwa mbaya.
    BINZUBEIRY ilishuhudia tiketi zilizouzwa leo ni za mechi ya Yanga na Azam ambayo ilifanyika Machi 26 mwaka huu.
    Tiketi hizo ni za Sh. 5,000 na jana ziliuzwa kiasi hicho hicho cha fedha lakini tarehe ikisomeka ni 6/4/2014.
    Awali mechi hiyo kabla ya kuahirishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  ilipangwa kuchezwa Aprili 6 mwaka huu.
    Katika mchezi huo wa raundi ya 24 Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kufikisha pointi 56 n kujiweka kwenye mazingira ya kuukaribia ubingwa wa Bara msimu huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KAMA SI UTAPELI HII TUITE NINI? MECHI YA RUVU NA AZAM WATU WALIPISHWA VIINGILIO MARA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top